Simba Yaipiga Bandari Ya Kenya Bao 1-0

Kikosi cha Simba kimeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Bandari FC ya Kenya katika mchezo wa kirafiki uliopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Bao pekee la mechi hiyo lilifungwa na Ibrahim Ajibu katika dakika ya 77 kipindi cha pili baada ya kupokea pasi kutoka kwa Rashid Juma.

Katika mchezo huo, Simba walikuwa na ufundi mwingi haswa katika kukontro mipira kuelekea katika lango la wapinzani ingawa mingi haikuwa na macho katika lango la Bandari.

Aidha, kipa Beno Kakolanya aliibuka shujaa baada ya kuokoa mashuti mengi kutoka wa wapinzani.


Toa comment