Kampuni ya ukuzaji Mchezo wa ngumi (PAF Promotion Entertainment Company Limited), imetangaza kuwa Bondia Hassan Mwakinyo sasa atapanda ulingoni kuwania ubingwa wa mkanda wa Mabara wa IBA dhidi ya Julius Munyelele Indongo kutoka Namibia badala ya Rayton Okwiri wa Kenya ambaye amepata majeraha akiwa mazoezini.
Tayari Julius Indongo yupo Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya pambano hilo na kesho Alhamisi Septemba 28, 2023 atakwepo kwenye viwanja vya Leader Club ambapo mabondia wote watakaoshiriki pambano hilo watapima uzito.
Shughuli za kupima uzito zitaanza saa 3:00 asubuhi huku pambano likitarajiwa kufanyika Ijumaa Septemba 29, 2023 kuanzia majira ya saa 12:00 jioni kwenye ukumbi wa Ubungo Plaza, Dar es Salaam.
Global Publishers and General Enterprises Limited is a registered private company dealing in publishing of weekly Swahili newspapers in Tanzania, namely; Uwazi, Ijumaa, Championi, Amani, Risasi & Ijumaa Wikienda.