Wateja wa Gas Fasta Sasa Kuagiza Gesi Kupitia Aplikesheni ya M-Pesa

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Patrobas Katambi (katikati) akiwa ameshikilia mfano wa mtungi wa gesi kuashiria uzinduzi rasmi wa upatikanaji wa huduma ya Gas Fasta kwenye M-Pesa Super App kupitia ushirikiano uliofanyika jijini Dar es Salaam. Pamoja naye kulia ni Mkurugenzi wa M-Pesa, Epimack Mbeteni na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Gas Fasta, Mohammed Albeiiti, kupitia ushirikiano huo unaolenga kurahisisha na kuhamasisha matumizi ya gesi asilia nchini, siku 30 za mwanzo, mteja atarudishiwa mpaka shilingi elfu kumi papo hapo pindi anunuapo gesi kupitia aplikesheni ya M-Pesa.

Wateja wa Vodacom Tanzania na Gas Fasta wamerahisishiwa upatikanaji wa gesi kupitia ushirikiano wa kampuni hizo mbili unao wawezesha kuagiza, kulipia na kisha kufikishiwa mitungi ya gesi kupitia aplikesheni ya M-Pesa.

Akizungumza wakati wa kuzindua rasmi ushirikiano huo, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Patrobas Katambi amepongeza jitihada zinaonyeshwa na sekta binafsi kwa kutumia ubunifu wao wa kidigitali katika kuunga mkono juhudi za serikali ambao utaongeza hamasa ya Watanzania kutumia gesi asilia na rafiki kwa utunzaji wa mazingira nchini kote.

“Niwapongeze M-Pesa na Gas Fasta kwa ushirikiano huu muhimu ambapo mmeamua kuunganisha nguvu kuwarahisishia Wateja wenu kupata huduma ya gesi kwa njia ya kidigitali. Tukio hili halitokuwa na manufaa kwa wateja wenu pekee pia na kwa Watanzania wote kwa ujumla kwa sababu wote wanapendelea upatikanaji wa huduma na bidhaa kwa usalama, uharaka, na unafuu kuendana na maisha yao ya kila siku.

Kama serikali, tunafanya jitihada kubwa kwa kushirikiana na wadau tofauti nchini kuongeza nguvu ya kujenga hamasa na kutoa elimu ya matumizi sahihi ya gesi asilia ambayo ni rafiki kwa utunzaji wa mazingira. Nitoe wito kwa ushirikiano wa namna hii katika maendeo mbalimbali ili kufikia malengo yetu ya Watanzania wote kutumia gesi asilia kwa manufaa ya afya na uchumi wa taifa lote kwa ujumla,” alisema Katambi.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mh. Patrobas Katambi akizungumza na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi rasmi wa upatikanaji wa huduma ya Gas Fasta kwenye M-Pesa Super App kupitia ushirikiano uliofanyika jijini Dar es Salaam. Wakimsikiliza jukwaani kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Gas Fasta, Bw. Bw. Mohammed Albeiiti pamoja na Mkurugenzi wa M-Pesa, Bw. Epimack Mbeteni, kupitia ushirikiano huo unaolenga kurahisisha na kuhamasisha matumizi ya gesi asilia nchini, siku 30 za mwanzo, mteja atarudishiwa mpaka shilingi elfu kumi papo hapo pindi anunuapo gesi kupitia aplikesheni ya M-Pesa.

Akielezea umuhimu wa ushirikiano na Gas Fasta uliozinduliwa jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa M-Pesa, Epimack Mbeteni amesema kuwa huu ni mwendelezo wa jitihada zao za kuifanya aplikesheni ya M-Pesa kujitosheleza na kuwawezesha Watanzania kuitumia kwa manunuzi na malipo ya huduma na bidhaa mbalimbali kwa kidigitali.

“Tunayo furaha kuwakaribisha Gas Fasta katika familia ya M-Pesa Super App. Kama tulivyowafahamisha wakati tukiizindua, lengo letu ni kuifanya M-Pesa kuwa sehemu ya maisha ya kila siku ya watanzania yaani ‘Digital Lifestyle App’ huku ikichochea mapinduzi ya uchumi wa kidijitali nchini.

“Hii ina maana kuwa siku zijazo wateja hawatokuwa na haja ya kuwa na utitiri wa aplikesheni za huduma tofauti katika simu zao, kwani M-Pesa pekee itajitosheleza kukidhi mahitaji yao. Ushirikiano wetu na Gas Fasta ni wa kipekee sana kwani unaenda sambamba na malengo yetu mapana kama Vodacom Tanzania kwenye utunzaji wa mazingira.

Vilevile kama hii haitoshi, katika siku 30 za mwanzo, mteja atarudishiwa hadi shilingi elfu kumi papo hapo pindi atakapofanya manunuzi ya gesi kupitia aplikesheni ya M-Pesa” alisema Bw. Mbeteni.

Aidha Mkurugenzi huyo alibainisha kwamba muundo wa M-Pesa wa uundaji wa thamani (yaani value creation model) umejikita katika kushirikiana na jamii zilizowazunguka pamoja na wadau mbali mbali katika kufanikisha utoaji wa huduma zao.

Falsafa hii imewawezesha kutengeneza ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja kwa watanzania takribani 1,000 pamoja na kushirikiana na taasisi za serikali na sekta binafsi katika malipo na makusanyo hivyo kuchochea ukuaji wa kiuchumi.

Mkurugenzi wa M-Pesa, Bw. Epimack Mbeteni akizungumza na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi rasmi wa upatikanaji wa huduma ya Gas Fasta kwenye M-Pesa Super App kupitia ushirikiano uliofanyika jijini Dar es Salaam. Wakimsikiliza jukwaani wa kwanza kulia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mh. Patrobas Katambi pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Gas Fasta, Bw. Bw. Mohammed Albeiiti, kupitia ushirikiano huo unaolenga kurahisisha na kuhamasisha matumizi ya gesi asilia nchini, siku 30 za mwanzo, mteja atarudishiwa mpaka shilingi elfu kumi papo hapo pindi anunuapo gesi kupitia aplikesheni ya M-Pesa.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Gas Fasta, Bw. Mohammed Albeiiti, amebainisha kuwa, “ni furaha na heshima ya kipekee kushirikiana na M-Pesa, huduma iliyoleta mapinduzi ya ujumuishaji wa huduma za kifedha nchini na ukanda wote wa Afrika ya Mashariki.

Huduma yetu ya Gas Fasta ilianzishwa baada ya kutambua usumbufu na upotevu wa muda na gharama wanaoupata Watanzania pindi wanapoishiwa na gesi, na mara nyingi wakati wakipika. Kama tunavyofahamu, huwezi kumwaga chakula au ukaenda kununua kingine pindi ukiishiwa na gesi, suluhisho ni kuagiza mtungi mwingine.

Na hapo ndipo sisi tulipokuja na suluhisho la kidigitali, kwa kutambua idadi kubwa ya watu wanatumia simu janja, tukaona ni fursa ya kuwafikia muda na mahali popote walipo kwa uhakika na usalama zaidi. Tuna matarajio makubwa kupitia ushirikiano huu na ukubwa wa M-Pesa kutokana na teknolojia, uzoefu na rasilimali zake hususani yanapokuja masuala ya kidigitali maana yenyewe ni huduma ya kidigitali na siku zote inafikiria kidigitali zaidi.”

Kupitia Gas Fasta, mtumiaji anaweza kufanya manunuzi ya gesi na kufikishiwa alipo kutoka kwa wasambazaji wote wa gesi za kupikia nchini na hivyo kuchangia utunzaji wa mazingira kupitia matumizi ya nishati safi ya kupikia. Hali kadhalika, kupitia aplikesheni ya M-Pesa, watumiaji wamewezeshwa kufanya manunuzi na malipo kwenda kwa watoa huduma takribani 20 ikiwemo tiketi za usafiri wa anga, vifurushi vya televisheni, malipo ya bidhaa kidogo kidogo na nyinginezo nyingi.


Football news:

<!DOCTYPE html>
Kane on Tuchel: A wonderful man, full of ideas. Thomas in person says what he thinks
Zarema about Kuziaev's 350,000 euros a year in Le Havre: Translate it into rubles - it's not that little. It is commendable that he left
Aleksandr Mostovoy on Wendel: Two months of walking around in the middle of nowhere and then coming back and dragging the team - that's top level
Sheffield United have bought Euro U21 champion Archer from Aston Villa for £18.5million
Alexander Medvedev on SKA: Without Gazprom, there would be no Zenit titles. There is a winning wave in the city. The next victory in the Gagarin Cup will be in the spring
Smolnikov ended his career at the age of 35. He became the Russian champion three times with Zenit

17:45 Chino ataweza kuleta ushindani kwenye lebo za muziki zilizopo??
17:43 Chino atangaza kufunngua lebo na kusaini wasanii, kuingiza kwenye upinzani wa lebo Tanzania
17:43 Chino atangaza kufunngua lebo na kusaini wasanii
15:53 Hii Ndiyo Mikataba 8 ya Ushirikiano Iliyosainiwa Kati ya Tanzania na Zambia
15:49 Taasisi ya Lalji Foundation Yaendesha Kambi ya Macho, 100 Wafanyiwa Upasuaji
15:20 Rais wa Zambia Ashukuru Rais Samia Kuipa nchi hiyo hekta 20 za ardhi
15:20 Rais Samia Awapa Hekta 20 Zambia Kujenga Bandari, Atua Ikulu ya Lusaka (Video+Picha)
14:28 Sloti ya Book of Egypt Chimbo la Utajiri Meridianbet
10:15 Waziri Mavunde: Tanzania Iko Tayari Kushiriki Uchumi wa Madini Ya Bahari
10:14 Wateja wa Gas Fasta Sasa Kuagiza Gesi Kupitia Aplikesheni ya M-Pesa
8:12 Fahamu namna msikiti wa Al-Aqsa ulivyochochea mzozo wa Israel na Palestina
11:03 ACT Wazalendo wamteua Dk. Suleiman kugombea Uwakilishi Jimbo la Mtambwe
9:19 Bajeti Ya Serikali Ya Marekani Chupuchupu Kukwama – Yapata Idhini Ya Matumizi Ya Wiki Sita Tu
9:16 Kuna Maisha Baada Ya Kutendwa Soma Hapa Ujinasue!
8:59 Mwanamume Afariki Baada ya Nyangumi Kugonga Boti
8:52 Chama, Luis Wapewa Zigo Zito Kuiondosha Power Dyhamos
8:41 Rais Samia akitangaza Chuo cha Diplomasia sasa kuitwa Dk. Salim Ahmed Salim
8:33 NIT kuanza kufundisha walimu wa ufundi
8:22 Papa Francis awapandisha vyeo makasisi 21 kuwa makadinali
8:14 Breaking: Moto Mkubwa Unateketeza Majengo Na Maduka Kariakoo, Dar – Video
4:31 Mama Wa Mapacha Aliyekuwa Amezuiwa Hosptalini Arusha Alipiwa Bili – Video
21:04 Wananchi Geita wachangamkia uchunguzi wa saratani bure, wanawake wapewa neno
15:24 Shirika la Ndege la Rwandair Lamwaga Zawadi Kwa Wateja, Wadau Wa Tanzania
9:22 #Exclusive: Neema Chande Afichua Alivyotoka Kimapenzi Na Romy Jons Na Kuzaa – Video
8:00 Anayedaiwa Kumuua Tupac Mwaka 1996 Akamatwa na Polisi
7:14 Basi la magereza lagonga treni, mmoja afariki, 10 wajeruhiwa
7:08 Wema Sepetu ajutia kilichotokea katika sherehe ya birthday yake “Sitafanya tena birthday”
6:35 Inasikitisha! Mume Alinikimbia Nikiwa Na Mimba, Nikaanza Penzi Na Mume Wa Mtu – Video
5:20 Rais Samia Ateua na Kuridhia uteuzi wa Viongozi Mbalimbali
5:03 Ukiingia Kwenye Ndoa na Mwenye Sifa Hizi, Huwezi Kujuta!
4:57 Basi la Magereza Lagonga Treni Yenye Abiria 650 Dar
4:57 Basi la Magereza Lagonga Treni Ya Abiria Ukonga Dar, Yasababisha Kifo cha Mtu Mmoja
3:18 “Utalindwa Usiogope Kutoa Ushahidi” – Waziri Pindi Chana Akizindua Miongozo…
2:55 Putin na Rais wa Sudan Kusini Wafanya Mazungumzo Mjini Moscow
2:00 Mchungaji Mwakipesile Ahukumiwa Kifungo Cha Miaka Mitatu Jela
1:05 Manchester United Yatangaza Yamrejesha Antony Kuendelea na Mazoezi
22:13 NIT yatakiwa kukamilisha miradi yake kwa muda uliopangwa
21:10 Magari taasisi za umma, binafsi zatakiwa kufanyiwa ukaguzi NIT
20:15 Tanesco Ubungo yatakiwa kushughulia tatizo la kukosekana kwa umeme
20:06 Naibu Waziri aipa Tanesco Ubungo saa sita kushughulia tatizo la kukosekana kwa umeme
17:37 Taja tofauti kati ya Ku-run game ya muziki na ku-hit kwenye muziki
17:27 EL Mando ataja orodha ya wasanii watano waliowahi kui-run game ya Bongo Fleva, amtoa Alikiba
17:20 Orodha ya wasanii watano waliowahi kui-run/kuiendesha game ya muziki wa Bongo Fleva
15:53 Dianne Feinstein, Seneta aliyetumikia kwa muda mrefu afariki akiwa na miaka 90
14:11 Mwalimu Mtanzania aingia top 50 ya Global Teacher Prize 2023
13:19 Naibu Waziri wa Nishati Aipa Saa Mbili Tanesco Kurudisha Umeme
12:49 Rais wa Rwanda Amteua Jenerali Mshukiwa kuwa Waziri
12:29 Viwanda Zaidi ya 200 Kuonyesha Bidhaa Maonyesho ya TIMEXPO Dar
11:26 Mapya Yaibuka Vijana Waliopotea Kariakoo Siku 373 -Wazazi Wao Wafunguka Haya – “Rais Samia Tusaidie”- Video
10:53 Mchengerwa Awatangazia Kiama Wakurugenzi Watakaoshindwa Kutekeleza Mradi wa TACTIC
9:39 Simba Watamba Kufuzu Makundi Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamos
9:26 Lulu Diva Amkataa Rich Mavoko – Afichua Kwa Nini Anachagua Andazi – “Ex Harudiwi” – Video
9:11 Kocha wa Yanga Atamba Kumaliza Kazi dhidi ya Al Merrikh ya Sudan
9:03 Sakata La Kupotea Kwa Warda – Mama Mkubwa Aangua Kilio Aomba Rais Samia Aingilie Kati – Video
8:19 Nina 5% za kupanda Ulingoni, epuka matapeli- Mwakinyo
3:30 Watu 6 wauwawa, 10 wajeruhiwa katika shambulizi Somalia
2:21 Habari Kubwa Za Magazeti Ya Tanzania Leo Ijumaa, Septemba 29, 2023
16:51 Nape; Tutumie mitandao ya kijamii kujiingizia kipato si kufanya umbea
15:44 Nyumbu SC yatoka sare na Polisi Tanzania mchezo wa kirafiki
8:25 Uganda Yawasimamisha Kazi Wafanyikazi 11 juu ya Vibali Bandia vya Sokwe
6:37 Madaktari wazawa waendelea kupandikizwa figo Muhimbili
6:12 Carabao Cup: Man United Yapangwa Kukipiga Na Newcastle United
6:08 Dk. Mpango kukutana na mashirika yasiyo ya Kiserikali takribani 9,000
5:50 Mkuu wa MINUSCA atembelea kikosi cha walina amani wa Tanzania Afrika ya Kati
5:19 Dkt. Biteko: Tutaleta Umeme Vijijini Hata Kama Wananchi Hawana Nyumba Nzuri
5:04 Yanga Yashtukia Mtego Wapinzani Wao Al Merrikh Ligi ya Mabingwa Afrika
5:02 Mbinu 5 za Kumbaini Mpenzi Mchepukaji
4:46 Simba Njia Nyeupe CAF Wachezaji Watatu wa Power Dynamos Kuukosa Mchezo
4:37 Jinsi ya Kumtambua Mwanaume wa Kukuoa!
4:22 Mwakinyo Abadilishiwa Mpinzani Kuzichapa Dhidi ya Mnamibia
4:15 Mkurugenzi Tanesco: Upungufu Wa Umeme Utamalizika Machi 2024 – Video
4:08 Dereva Bajaji Apotea Vingunguti Hofu Yaikumba Familia | Katambuga – Video
1:58 Habari Kubwa Za Magazeti Ya Tanzania Leo Alhamisi, Septemba 28, 2023
19:10 Wasanii waliopo Kings Music, Konde Gang, Next level hawatengenezi hela kupia muziki wao
19:06 Harmonize, Alikiba, Rayvanny na Nandy hawajafanya uwekezaji wa kutosha kwenye lebo zao
18:53 Lebo nyingi Tanzania zimewatelekeza wasanii wao
14:24 Muimbaji E Major aachia Jara (Video)
13:22 Mwakinyo abadilishiwa mpinzani wa pambano lake
11:00 Kocha Roberto Oliveira ‘Robertinho’ Aipeleka Simba Mafichoni
10:44 Tamwa: Rushwa ya ngono kikwazo wanahabari wanawake kushika nafasi za juu za uongozi
8:41 Moto Iraq: Maharusi Wote Wawili Wapoteza Maisha, Afisa wa afya Afunguka
8:32 Mbinu za Kumfanya Aamini Kama Kweli Unampenda kwa Vitendo
7:30 Baleke Anautaka Ufungaji Bora Ligi Kuu Bara msimu huu
7:07 #Exclusive: Aunty Ezekiel – “Wolper Ananipendana Sana – Siamini Mitandao Mpaka Nione Kwa Macho”- Video
5:52 Gamondi Aandaa Silaha mpya Yanga dhidi ya Al Merrikh Azam Complex, Dar
5:38 IRAQ: Moto Waua Watu 100 Kwenye Harusi, Bibi Harusi na Bwana Harusi Wadaiwa Kufariki – Video
5:19 Trump adaiwa kufanya udanganyifu wa kibiashara kwa miaka mingi
2:30 Habari Kubwa Za Magazeti Ya Tanzania Leo Jumanne, Septemba 27, 2023
1:20 Rais Samia: Tuna ‘Crisis’ Ya Umeme, Tunafanya Ukarabati Wa Mashine – Video
23:37 Rais Samia agundua Maharage ana biashara TTCL
23:34 Mkurugenzi Tanesco apewa miezi sita katikakati ya umeme
23:30 Tanzania, Marekani kushirikiana kuboresha mifumo ya usimamizi masuala ya afya
15:44 VIDEO: Infinix Zero 30 yatua TZ, Director Kenny anogewa
14:21 Simba Yatamba Kuwashangaza Power Dynamos Kutinga Hatua ya Makundi
12:00 Marekani imemkatalia waziri wa mambo ya nje wa Iran, kutembelea Washington
11:49 Staa wa TikTok akamatwa na Polisi kwa kudangaya Umma mlevamu
10:16 Tanzania nashika nafasi ya 9 kwenye mataifa yasiyokuwa na furaha duniani
9:52 Man United: Sancho Apigwa Marufuku Kutumia Mgahawa Wa Kikosi Cha Kwanza
9:40 Mjukuu wa Nelson Mandela, Zoleka Afariki Familia yake Yatangaza
9:13 Winga ashusha presha Simba Kurejea Uwanjani Baada ya Wiki Moja