Wasomaji Wa Championi Na Spoti Xtra Wazidi Kuchangamkia Gari

Wasomaji wa magazeti ya bora ya michezo, Championi na Spoti Xtra, leo Jumamosi wamezidi kuchangamkia shindano la kubwa la Baba lao ambapo mshindi anatarajiwa kuondoka na gari mpya aina ya Fun Cargo.

Kitengo cha Masoko na Usambazaji cha magazeti hayo, leo kilizunguukia maeneo mbalimbali ya jiji la Dar ikiwemo Ubungo Survey, Makongo Juu na Goba ambapo na kuuza na magazeti hayo na kuendelea kulitangaza shindano hilo.

Wasomaji walipitiwa na kikosi hicho walionekana kulichangamkia gazeti la Championi Jumamosi walilokuwa wakiliuza maeneo hayo na kujaza kuponi kwa ajili ya kujishindia gari hilo.

Akizungumza na wasomaji hao, Mkuu wa Idara ya Masoko na Usambazaji, Anthony Adam aliwahamasisha wasomaji wa magazeti ya michezo kununua magazeti hayo yanayoongoza kwa kuandika habari za uhakika.

Pamoja na kununua na kusoma magazeti hayo, Anthony aliwasisitiza wasomaji hao kuchana kuponi iliyopo ukurasa wa pili kwenye magazeti hayo na kumkabidhi muuza magazeti yeyote aliye karibu nao kwa ajili ya kuweza kujishindia gari hilo.

Anthony aliendelea kusema kuwa katika kuelekea kwenye shindano hilo, Ijumaa ijayo itachezeshwa droo ndogo ambapo washindi wanatarajiwa kuibuka na zawadi mbalimbali ikiwemo simu janja (smart phone) na zawadi nyinginezo. Alisema Anthony alipokuwa akizungumza na wasomaji hao.

Stori Na Richard Bukos

Toa comment