Tanzania
This article was added by the user . TheWorldNews is not responsible for the content of the platform.

Baleke Anautaka Ufungaji Bora Ligi Kuu Bara msimu huu

Jeane Baleke

MSHAMBULIAJI wa Simba, Mkongomani, Jeane Baleke, ameahidi kuendelea kufunga mabao katika kila mchezo ili afanikishe malengo yake ya kufikisha mabao zaidi ya 20 ndani ya Ligi Kuu Bara msimu huu na kuwa mfungaji bora.

Kauli hiyo imekuja ikiwa ni siku chache zimepita, tangu apige hat trick katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Coastal Union, uliochezwa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Akizungumza na Spoti Xtra, Baleke mwenye mabao matano katika Ligi Kuu Bara msimu huu, alisema msimu uliopita alishindwa kufikisha idadi hiyo ya mabao, kutokana na kujiunga na timu katikati ya msimu.

Baleke alisema anaamini malengo yake yatafanikiwa ya kuchukua ufungaji bora, kama akiendelea kupata ushirikiano kutoka kwa wenzake na asipopata majeraha.

Aliongeza kuwa, licha ya ugumu wa ligi uliokuwepo, lakini hiyo haimfanyi ahofie malengo yake kutotimia msimu huu, atahakikisha anatumia vema kila nafasi atakayoipata.

“Binafsi natamani kuona nikifunga mabao kuanzia 20 kwenye ligi msimu huu, huku nikiamini yatatosha kuisaidia Simba kutwaa ubingwa.

“Nafahamu ugumu wa ligi ambao tayari nimeuzoea kwa miezi sita niliokuwepo hapa Simba, hivyo nimejipanga vema kupambana na timu yoyote nitakayokutana nayo katika ligi,” alisema Baleke.

STORI NA WILBERT MOLANDI

spoti pesa below post

Global Publishers and General Enterprises Limited is a registered private company dealing in publishing of weekly Swahili newspapers in Tanzania, namely; Uwazi, Ijumaa, Championi, Amani, Risasi & Ijumaa Wikienda.