Tanzania
This article was added by the user . TheWorldNews is not responsible for the content of the platform.

Kocha Roberto Oliveira ‘Robertinho’ Aipeleka Simba Mafichoni

Global Publishers and General Enterprises Limited is a registered private company dealing in publishing of weekly Swahili newspapers in Tanzania, namely; Uwazi, Ijumaa, Championi, Amani, Risasi & Ijumaa Wikienda.

KUANZIA wiki hii, kikosi cha Simba chini ya Kocha Roberto Oliveira ‘Robertinho’, kimepanga kuutumia Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, Mbagala, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya kufanya mazoezi ya mwisho kuelekea mchezo dhidi ya Power Dynamos ya Zambia.

Timu hizo zitavaana katika mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Afrika utakaochezwa Jumapili hii ukiwa ni wa marudiano.

Katika mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Levy Mwanawasa, Ndola nchini Zambia, timu hizo zilitoka sare ya kufungana mabao 2-2.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra, Simba wameomba kutumia uwanja huo, maalum kwa ajili ya wachezaji kuuzoea kabla ya kukabiliana na Power Dynamos.

Mtoa taarifa huyo alisema walitarajiwa kuanza kuutumia uwanja huo jana Jumatatu kuanzia saa moja usiku muda ambao watautumia kuucheza mchezo wao dhidi ya Power Dynamos, kuwania kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Aliongeza kuwa, tayari uongozi wa Simba umewasilisha barua kwa menejimenti ya Azam kwa ajili ya kuutumia uwanja huo kufanyia mazoezi.

“Kuanzia wiki hii yote, Simba itafanya mazoezi yake ya mwisho kwenye Uwanja wa Azam Complex kuelekea mchezo wa marudiano dhidi ya Power Dynamos.

“Lengo kubwa likiwa ni wachezaji kuuzoea uwanja huo ambao una nyasi bandia, kwani uwanja huo ndio tutakaoutumia katika mchezo wa marudiano.

“Kikubwa tunataka kuona timu yetu ikifuzu hatua ya makundi, hivyo ni lazima tukiandae kikosi chetu kwa kutimiza baadhi ya mahitaji muhimu,” alisema mtoa taarifa huyo.

Mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu, alithibitisha hilo kwa kusema: “Kuanzia wiki hii kikosi chetu kitakuwa kikifanya mazoezi Uwanja wa Azam Complex, kwani mechi yetu dhidi ya Power Dynamos inachezwa hapo.”

spoti pesa below post