Tanzania
This article was added by the user . TheWorldNews is not responsible for the content of the platform.

NIT yatakiwa kukamilisha miradi yake kwa muda uliopangwa

NAIBU Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile amekitaka Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kukamilisha miradi yake yote kwa muda uliopangwa sambamba na kuhakikisha thamani ya fedha.

Akizungumza jijini Dar es Salaam mara baada ya kutembelea miradi mbalimbali ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Kihenzile amesema pia anakielekeza Chuo hicho kuongeza hosteli nyingi ili kuchukua wanafunzi wengi na kupunguza changamoto ya wengine kupanga nje ya shule ambako hakuna mazingira rafiki.

Amesema idadi ya wanafunzi katika chuo hicho inaongezeka na sasa imefikia 15,000 na kwamba wanatarajia wanafunzi wengi zaidi.

Kwa upande wake, Mkuu wa chuo hicho, Profesa Zakaria Mganilwa amesema wana miradi ya ujenzi wa majengo ya kufundishia pamoja na hosteli na kwamba watahakikisha miradi hiyo inamalizika kwa muda uliopangwa na ubora unaotakiwa.

Amesema chuo kina mshauri mwelekezi pamoja na wataalamu wa ujenzi ambao wamewashiiza katika miradi hiyo na kwamba wanamsimamia mkandarasi kufanya kazi kwa ubora unaotakiwa

kituo cha ukaguzi wa magari kilijengwa kwa ajili ya wanafunzi wao, maofisa wa polisi wanaohusika na ukaguzi na maofisa wa bima.

Amesema wanachokifanya maofisa wa bima ni kuthamanisha gari baada ya kupata ajali na kisha kuwalipa wateja wao.

“Tumekuwa tukihamasisha umma walete magari yao Ili kujua ubora wake kwani tunakagua zaidi ya mifumo 15 hasa inayoendana na usalama wa gari,”amefafanua.

Profesa Mganilwa amesema watu ambao wanauziana magari pia Wana wajibu wa kupeleka magari hayo kufanyiwa ukaguzi kabla ya kununua ili likaguliwe na watapewa taarifa ya gari husika.

“Baada ya ukaguzi tutatoa ripoti ambayo huenda mnunuzi badala ya kununua kwa Shilingi milioni nane unaweza kuambiwa gari inahitaji matengenezo ya milioni 12 hivyo ukajikuta unanunua gari kwa milioni 20,” amesisitiza.

Amesisitiza kuwa wanahamasisha watanzania watumie kituo hicho kwani ukaguzi wa gari dogo huanzia Sh 60,000 huku gharama ya magari makubwa hutegemea na mahitaji na kwamba kituo hicho kitawasaidia kuwa na uhakika wa kupunguza ajali za barabarani.