Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kituo cha Ubungo kimepewa saa sita kuhakikisha wanashughulikia tatizo la kukosekana kwa umeme.

Hayo yamebainishwa leo na Naibu Waziri wa Nishati, Judithi Kapinga wakati akitoa maelekezo kwa watendaji wa shirika hilo mara baada ya kutembelea na kukagua mitambo ya umeme iliyopo Ubungo jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri Kapinga amesema anafahamu kuwa kituo cha Ubungo 1 kilizimika umeme tangu jana usiku huku jitihada za kurejesdha uzalishaji zikiendelea hivyo wananchi wasiwe na wasiwasi.

Amesema kwenye kituo hicho cha Ubungo 1 kuna mashine tat una mbili ndizo zinafanya kazi huku moja haifanyi kazi na ipo kwenye matewngenezo.

“Kituo cha Ubungo 2 kina mashine 12 na sita kati ya hizo hazifanyi kazi ziko kwenye matengenezo lakini hizo sita zinazofanya kazi ndio zimezimika,” amesema Naibu Waziri Kapinga

Aidha amesema kuwa mashine zilizoharibika zina uwezo wa kuzalisha umeme wa Megawati 43 kila moja, ni umeme mwingi sana hivyo wanaimani kuwa kama matengenezo yatakamilika kwa wakati hali ya upatikanaji wa umeme itaimarika.

Photo of Yasini Ngitu

Related Articles