Tanzania
This article was added by the user . TheWorldNews is not responsible for the content of the platform.

Harmonize, Alikiba, Rayvanny na Nandy hawajafanya uwekezaji wa kutosha kwenye lebo zao

Kupitia kweye kipindi chake cha RECAP & MANDO @el_mando_tz ameweka wazai kuwa wamiliki wa lebo za Kings Music ambaye ni Alikiba, Konde Gang ambaye ni Harmonize, Next Level ambaye ni Rayvanny, The African princes ambaye ni Nandy hawajafanya uwekezaji wa kutosha kwenye lebo zao.

Asilimia kubwa wameanzisha lebo kama sifa tu kuonekana wanamiliki lebo lakini kwenye ukweli uendeshaji wa hizo lebo umewashinda na matokeo yanaonekana hadharani hayajifichi.

Kwa sasa wasanii wengi ukiwauliza kama wanataka kuingia kwenye lebo za muziki watakataa kwa sababu hawaoni kinachofanyika kwenye baadhi ya lebo za muziki nchini Tanzania.

Wamiliki wa lebo hizo wanaonekana kama wamezisusa lebo zao, wasanii wao wanaonekana kupitia magumu sana kwenye career zao za kimuziki.

Ukifuatilia msanii mmoja mmoja unaona kabisa hawakui kimuziki bali wanashuka kila mwaka kimuziki, hii inaleta picha mbaya sana kwenye career zao za muziki, na sio ajabu ukiwauliza kati ya kubaki kwenye lebo au kuondoka watachagua kuondoka kwenye lebo zao.

Sapoti wanayopewa na maboss zao ni ndogo sana na huenda hawakutegemea hicho, siku hizi wasanii wasiokuwa kwenye lebo wanafanikiwa zaidi kuliko waliopo kwenye lebo na sabbau kubwa ni uwekezaji wa wamiliki wa hizo lebo.

Unakubaliana na @el_mando_tz kwa asilimia ngapi??