Tanzania
This article was added by the user . TheWorldNews is not responsible for the content of the platform.

Mkuu wa MINUSCA atembelea kikosi cha walina amani wa Tanzania Afrika ya Kati

MKUU wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda Amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (MINUSCA), General Haphurey Nyone amefanya ziara ya kutembelea vikosi kikiwemo Kikosi cha Sita cha Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania (TANBAT6).

Nyone alitembelea kikosi hicho ambacho kinahudumu chini ya ujumbe wa MINUSCA ili kujitambulisha kwa mara ya kwanza tangu ashike nafasi hiyo.

Akitoa taarifa kwa umma akiwa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, Ofisa Habari wa kikosi hiyo, Kapteni Mwijage Inyoma alisema ziara hiyo ilianza kwa kupokelewa kwa Mkuu huyo pamoja na Kamanda wa kikosi cha TANBAT 6 Luteni Kanali Ramadhani Shaaban katika uwanja wa ndege wa Beriberati Mambere Kadei kisha kupigwa kwa gwaride la heshima.

Kapteni Inyoma alisema baadaye kiongozi huyo aliongozana na wanadhimu kutoka Makao makuu ya MINUSCA mjini Bangui ambapo huko alipata fursa ya kuongea na askari ambapo aliwasisitiza nidhamu, umoja na mshikamano bila kusahau kuwa na mahusiano mazuri na raia.

“Askari mila na desturi yake ni nidhamu na kufuata maelekezo, hapa nilipo nimempata taarifa kutoka kwa kamanda wa kikosi hiki Luteni Kanali Ramadhani jinsi mnavyo jituma katika utendaji kazi wenu, nimefurahi sana kusikia hivyo aidha hii ni kweli kwamba kikosi hiki kinasaidia vyema katika kutekeleza na kukamilisha jukumu la MINUSCA hapa Jamhuri ya Afrika ya kati, ninawasii kuendeleza hivyo bila kusahau kuzidi kuepuka suala zima la SEA”

Akitoa shukurani zake na za kikosi cha TANBAT6, Luteni kanali Ramadhani amesema kuwa amempokea kwa furaha Mkuu huyo kutembelea eneo lake la uwajibikaji , lakini pia kuona utimamu na utayari wa kikosi hicho kilichopo chini ya MINUSCA na kuahidi kudumisha aliyoelekezwa katika katika utendaji wa kikosi cha sita

Written by Janeth Jovin