Tanzania
This article was added by the user . TheWorldNews is not responsible for the content of the platform.

Chama, Luis Wapewa Zigo Zito Kuiondosha Power Dyhamos

Global Publishers and General Enterprises Limited is a registered private company dealing in publishing of weekly Swahili newspapers in Tanzania, namely; Uwazi, Ijumaa, Championi, Amani, Risasi & Ijumaa Wikienda.

KUELEKEA mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamos, Kocha Mkuu wa Simba, Roberto Oliveira ‘Robertinho’, amewapa majukumu mazito viungo wa timu hiyo wakiongozwa na Clatous Chama, Luis Miquissone na Fabrice Ngoma.

Simba ina kibarua cha kwenye mchezo wa leo ili kufuzu hatua ya makundi, baada ya ugenini ubao kusoma sare ya mabao 2-2.

Robertinho ameliambia Spoti Xtra kuwa, wachezaji wake wote kuanzia safu ya kiungo, ushambuliaji na ulinzi ni muhimu kufanya kazi kubwa ya kutafuta ushindi ndani ya dakika 90.

“Kwenye mpira kuna makosa ambayo yanafanyika, hayo kwetu tulifanyia kazi na tuliongea na wachezaji wote ikiwa ni pamoja na safu ya kiungo kupunguza makosa na kutumia makosa ya wapinzani kwa faida.

“Unaona kwenye eneo la kiungo kuna wakati kuna mipira ilikuwa inapotea kabla ya kufika mahali ilipotakiwa. Kwa kuzingatia hilo, viungo wanapaswa kuongeza umakini na washambuliaji nao katika kuzitumia nafasi ambazo tutazipata.

“Ulinzi kwetu ni muhimu kuwa imara hasa mwanzo mpaka mwisho. Unaweza ukapata bao kisha ukaruhusu hapo inakuwa kazi nyingine kwenye kutafuta ushindi. Ambacho kinanifurahisha ni utayari wa wachezaji katika kutimiza majukumu yao.

“Simba kucheza hatua ya makundi sio malengo bali ni hatua ambayo tayari imekuwa ni kawaida, lakini huwezi kucheza fainali kama utashindwa kushinda katika hatua kama hii na kisha ukavuka, wachezaji wangu wapo tayari kufanikisha hili jambo,” alisema Robertinho.

STORI NA LUNYAMADZO MLYUKA NA MARCO MZUMBE

spoti pesa below post