Tiktoker Maarufu kutoka nchini Ghana anayejulikana kwa jina la Kakai Shatta Aamekamatwa na polisi kwa kudaganya mlemavu kumbe sio mlemavu.

Vyombo vingi vya habari kutoka nchini Ghana vinaeleza kwamba Kakai Shatta amewadharau Waghana wengi kwa kujifanya kama mtu asiyejiweza ambapo imepelekea mpaka   kuchukua pesa kutoka kwa baadhi ya Waghana ambao hawajui.

Kakai Shatta aliwahi kwenda kwenye tv ya Onua (Televisheni ya Taifa) kuwahadaa Waghana kwa kuwaambia Waghana kuwa yeye ni mlemavu jambo ambalo si kweli anafanya hivyo kujichukulia pesa pia kwa ajili ya kuwa maarufu zaidi.

Baada ya matukio yake kuombva pesa akidanganya kuwa mlemavu inaelezwa kuwa wa wengi wanaomjua walianza kumripoti Polisi kwa Huduma ya Polise ya Ghana ili akamatwe na iwe fundisho kwa wengine.

Jumamosi tarehe 23 Septemba 2023 katika soko la Kaneshie Kakai Shatta alipokuwa akichukulia video kwa ajili ya kupost TikTok mbele ya mashabiki wake kwenye soko hilo inaelezwa ghafla polisi wa Kaneshie walimmkamata na sasa yupo Polisi.

Photo of Ally Juma