Taarifa ya TRC kuhusu ajali iliyotokea Dar na kusabanisha kifo cha mtu mmoja

“Shirika la Reli Tanzania – TRC linautaarifu umma kuwa Basi lenye namba MT 0040 mali ya
Jeshi la Magereza limegonga treni ya abiria namba D16 yenye injini namba 9015 iliyokuwa ikitokea mikoa ya Bara (Morogoro, Dodoma, Tabora na Kigoma) eneo la Ukonga jijini Dares Salaam, majira ya saa 11:25 jioni.

Ajali imehusisha basi la Magereza lililobeba wat 15, lililokuwa likivuka reli eneo la Kilomita 13 (Ukonga Magereza) a treni namba YD16 yenye injini namba 9015 ilivobeba abiria 650.

Ajali imesababisha kifo cha mtu mmoja na majeruhi 10, wanawake 5 a wanaume 5.
Majeruhi wamewahishwa katika Hospitali ya Amana kwa ajili ya matibabu.

Shirika linaendelea kuwashi madereva wa vyombo vya moto kuwa makini wanapokatiza reli kwa kufuata Sheria na alama za usalama wa reli zilizowekwa ili kuepusha ajali. Shirika linatoa pole kwa ndugu wa marehemu a Mwenyezi Mungu awape nafuu majeruhi ili waweze kuendelea na shughuli za kujenga taifa, taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.,”

Source: TRC

Photo of Yasini Ngitu