Tanzania
This article was added by the user . TheWorldNews is not responsible for the content of the platform.

Rais Samia Ateua na Kuridhia uteuzi wa Viongozi Mbalimbali

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameteua na kuridhia teuzi za viongozi mbalimbali kama ifuatavyo;

Amemteua Joel Laurent kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (Tanzania Fertilizer Regulatory Authority – TFRA).
Kabla ya uteuzi Laurent alikuwa Mhadhiri, Shule ya Sheria kwa Vitendo (Law School of Tanzania).

Ameridhia uteuzi wa Patrick Mongella kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (Cereals and Other Produce Board – CPB).
Mongella ni Mkurugenzi wa Miradi, Benki ya Maendeleo TIB.

Ameridhia uteuzi wa Mwanahiba Mohamed Mzee kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pembejeo za Kilimo (Agricultural Inputs Trust Fund – AGITF). Mwanahiba aliwahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank Tanzania.

Ameridhia uteuzi wa Irene Mlola kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na mazao Mchanganyiko (Cereals and Other Produce Regulatory Authority – COPRA). Mlola aliwahi kuwa Mkurugenzi Mku wa Financial Sector Deepening Trust (FSDT).

Ameridhia uteuzi wa Dkt. Andrew Komba kuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (National Food Reserve Authority – NFRA). Komba ni Mkurugenzi wa Mazingira, Ofisi ya Makamu wa Rais.

Ameridhia uteuzi wa Felix Mlaki kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ranchi za Taifa (National Ranching Company Limited – NARCO). Mlaki ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya NARCO.

spoti pesa below post

Global Publishers and General Enterprises Limited is a registered private company dealing in publishing of weekly Swahili newspapers in Tanzania, namely; Uwazi, Ijumaa, Championi, Amani, Risasi & Ijumaa Wikienda.