Tanzania
This article was added by the user . TheWorldNews is not responsible for the content of the platform.

NIT kuanza kufundisha walimu wa ufundi

MKUU wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Profesa Zacharia Mganilwa amesema kuwa chuo hicho kinakwenda kuanza kufundisha walimu wa masuala ya ufundi ambao watahitajika katika shule za sekondari nchini ili kufundisha mafunzo ya amali.

Mganilwa amesema kutokana na kuanza kwa mtaala mpya wa mafunzo hayo ya amali ambayo yamegawanyika katika fani 15 ikiwemo uhandisi umeme, mitambo, ujenzi, magari na huduma za usafirishaji chuo hicho sasa kitaanza kutoa kozi ya ufundi kwa walimu wote wanaopenda kusomea fani hiyo.

Hayo aliyabainisha jana jijini Dar es Salaam na Profesa Mganilwa wakati wa hafla fupi ya kuliaga baraza la uongozi la 11 na kukaribisha la 12, chuoni hapo.

Alisema mafunzo hayo ya amali yiataanza kidato cha kwanza hivyo kutakuwa na uhitaji wa walimu wa ufundi, hivyo NIT kinakwenda kuanza kufundisha walimu wa ufundi ambao watahitajika katika shule za sokondari ambazo zitakuwa na mkondo wa amali lakini wataweza kutumika kufundisha watu wengine wa masuala ya ufundi.

Mwenyekiti wa Baraza la 12 la Uongozi wa Chuo, Prof. Ulingeta Obadiah Mbamba akizungumza katika hafla ya kuliaga Baraza la Uongozi la 11 lililomaliza muda wake, hafla ambayo imefanyika leo Septemba 30,2023 Jijini Dar es Salaam.

“Naamni baraza la 12 zitahakkisha suala hilo ambalo lilianzishwa na kusimamiwa na baraza la 11 linakwenda kutekelezwa kwa wakati,” alisema

Aidha alisema bado kuna gharama kubwa ya kusomesha wataalam na wabobezi wa usafirishaji nje ya nchi huku akitolewa mfano kusomesha rubani nchini Afrika kusini nu sh, miliomi 300.

“Kwa juhudi tunazozifanya tutakapoanza kufundisha marubani hapa nchini gharama itakuwa Milioni 70 hivyo itapunguza makali,” alisema Profesa Mganilwa.

Hata hivyo Profesa Mganilwa alisema uanzishwaji wa Kituo cha Mafunzo ya Usalama Barabarani ambacho kinafadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika kwa gharama ya Sh. Bilioni 49 ni moja ya mafanikio yaliyopatikana katika Uongozi wa Baraza la 11.

“Kutokana na wingi wa matukio ya ajali barabarani, kituo hiki kimedhamiria kupunguza ajali za barabarani”. alisema Profesa Mganilwa

Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi Jipya la 12 Dkt.Dina Zawadi Machuve (kulia) akipokea vitendea kazi kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la 11 lililopita Mhandisi Dkt. Gemma Modu katika hafla ya kuliaga Baraza la Uongozi la 11 lililomaliza muda wake.

Kwa upange wake wa Baraza la 12 la uongozi wa chuo hicho, Profesa, Ulingeta Mbamba alisema baraza hilo litahakikisha linafanya kazi kwa kadri inavyowezekana.

Alisema Serikali imewekeza kwa kiasi kikubwa kwenye miundombinu ya usafirishaji, hivyo hata wao hawana budi kufanya kazi ya ziada katika kuhakikisha wanaunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali kwenye sekta ya usafirishaji.

Aidha ameishukuru menejimenti ya Chuo cha Taifa Cha Usafirishaji (NIT) kwa kuendelea kufanya vizuri, hivyo baraza lipo kwaajili ya kusaidia na maendeleo yaweze kuonekana zaidi.

Naye, Mjumbe wa Baraza la 11 la Uongozi wa Chuo, Mhandisi Eliona Simbo, akiongea kwa niaba ya Wajumbe wa Baraza , alisema kwa kipindi walichokuwepo walipata ushirikiano mkubwa na menejimenti ya Chuo hivyo kufanya kuonekana kwa maendeleo chuoni hapo

“Haya maendeleo yanayoonekana, hatuna budi kuishukuru menejimenti ya Chuo kwa ushirikiano mkubwa walioutoa pindi tunapoingia kazini kwa mara ya kwanza hadi kufikia mwisho na kuchaguliwa kwa Baraza lingine”. alisema

Written by Janeth Jovin