Tanzania
This article was added by the user . TheWorldNews is not responsible for the content of the platform.

Fahamu namna msikiti wa Al-Aqsa ulivyochochea mzozo wa Israel na Palestina

Kundi la wapiganaji wa Palestina ‘Hamas’ liliita shambulio lao la kushtukiza dhidi ya Israeli kama operesheni “Dhoruba ya Al Aqsa”. Msikiti wa Al Aqsa huko Jerusalem kihistoria umekuwa kitovu cha mvutano kati ya Wayahudi na Waislamu.

Msikiti huo kwa sasa uko chini ya udhibiti wa Jordan chini ya mkataba wa amani na unasimamiwa na Wakfu wa Trust nchini humo.

Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina Mahmoud Abbas anahusisha uchokozi wa Israel na maeneo muhimu ya Uislamu, kama vile Al Aqsa, kuwa sababu kuu ya hali ya sasa.

Hata hivyo, serikali ya Israel imekuwa ikikanusha madai hayo.

Rais Mahmoud Abbas kimsingi anatawala Ukingo wa Magharibi na hana mamlaka juu ya Gaza.

Mvutano unaoendelea kati ya Waarabu na Waisraeli ulifikia kilele mwaka huu wakati polisi wa Israel walipoingia kwa nguvu katika eneo la msikiti huo na kujaribu kuwafurusha waumini.

Israel inadai polisi waliingia katika eneo la msikiti huo kuwakamata Waislamu waliotambuliwa kama “wakatili”.

Picha nyingi za mapigano hayo ziliposambaa, kulizuka hisia kali katika ardhi za Palestina na ulimwengu mzima wa Kiislamu.

Tukio hilo lilitokea wakati wa mwezi mtukufu wa Waislamu wa Ramadhani na usiku wa kuamkia sikukuu ya kidini ya Kiyahudi ‘Pasaka ya Kiyahudi’.

Hapa historia ya Msikiti wa Al Aqsa inahitaji kuelezwa.

Suala hili limekuwa muhimu sana tangu shambulio la Hamas dhidi ya Israel na Israel kukabiliana na mashambulizi katika Ukanda wa Gaza.

Sikuliza Makala hiyo chini