Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa moja ya sababu ya kumuhamisha aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Maharage Chande kuwa Postamasta Mkuu Shirika la Posta Tanzania baada ya kugundua ana biashara ndani ya TTCL.

Rais Samia ameyasema hayo leo Septemba 26, 2023 wakati akiwaapisha viongozi mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam.

Amesema amemtoa Chande Tanesco na akachukua uzoefu wake angeweza kuiongoza TTCL lakini amegundua kuwa kiongozi huyo ana biashara ndani ya TTCL.

Hivi karibuni Rais Samia alimteua Chande kuwa Mkurugenzi wa TTCL akitokea Tanesco lakini ndani ya saa 48 akamhamisha tena na kumteua kuwa Postamasta Mkuu akichukua nafasi ya Macrice Mbodo ambaye atapangiwa nafasi nyingine.

Written by Janeth Jovin

Photo of Yasini Ngitu

Related Articles