Tanzania
This article was added by the user . TheWorldNews is not responsible for the content of the platform.

Simba Njia Nyeupe CAF Wachezaji Watatu wa Power Dynamos Kuukosa Mchezo

IMEFAHAMIKA kuwa, jumla ya wachezaji watatu tegemeo wa Power Dynamos ya nchini Zambia, wanatarajiwa kuukosa mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Simba.

Timu hizo zinatarajiwa kurudiana Jumapili ya wiki hii kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar, baada ya mchezo wa kwanza ugenini kutoka sare ya mabao 2-2.

Taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra, kutoka katika moja ya Jarida la Zambia, Power Dynamos itawakosa wachezaji wake muhimu katika kikosi cha kwanza kutokana na majeraha.

Wachezaji hao wawili watakosekana kutokana na majeraha waliyoyapata katika mchezo wa Ligi Kuu ya Zambia waliocheza wiki iliyopita dhidi ya Zesco United.

Jarida hilo liliwataja wachezaji hao ni, kipa namba moja Lawrence Mulenga na beki Aron Katebe ambao wote wanauguza majeraha.

Mwingine ni beki Dominic Chanda ambaye yeye anaitumikia adhabu ya kadi nyekundu.

“Power Dynamos FC imethibitisha rasmi kwamba kuelekea katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Simba, itakosa huduma kutoka kwa baadhi ya wachezaji wao muhimu wa kikosi cha kwanza kutokana na majeraha na adhabu ya kadi nyekundu.

“Wachezaji hao ni kipa Lawrence Mulenga aliyeumia katika mchezo dhidi ya Zesco United, beki Dominick Chanda ambaye ana majeraha,” ilisema sehemu ya taarifa ya jarida hilo.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, alizungumzia hilo kwa kusema: “Hivi sasa hatuwaangalii wapinzani wetu nini wanafanya, badala yake tunaelekeza nguvu zetu katika maandalizi ya kikosi chetu.

“Sisi katika mchezo huo, tutawakosa baadhi ya wachezaji wetu kama Kramo (Aubin), Manula (Aishi) na Inonga (Hennock) wenye majeraha.”

STORI NA WILBERT MOLANDI

spoti pesa below post