Tanzania
This article was added by the user . TheWorldNews is not responsible for the content of the platform.

Basi la Magereza Lagonga Treni Yenye Abiria 650 Dar

BASI  la Magereza lenye namba MT 0040 limegonga treni ya abiria namba YD16 yenye injini namba 9015 iliyokuwa ikitokea mikoa ya Bara (Morogoro, Dodoma, Tabora na Kigoma) katika eneo la Ukonga jjini Dar es Salaam, muda wa saa 11:25  Ijumaa jioni.

Basi hilo la Magereza lililokuwa limebeba watu 15 liliigonga na treni namba YD16 yenye injini namba 9015 iliyobeba abiria 650 wakati basi hilo likivuka reli eneo la Kilomita 13 (Ukonga Magereza).

Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano kutoka Shirika la Reli Tanzania, Jamila Mbarou imesema ajali hiyi imesababisha kifo cha mtu mmoja na majeruhi 10 ambao kati yak wanawake watano na wanaume watano.

Amesema majeruhi wamewahishwa katika Hospitali ya Amana kwa ajili ya matibabu.

“Shirika linaendelea kuwasihi madereva wa vyombo vya moto kuwa makini wanapokatiza reli kufuata Sheria na alama za usalama wa reli zilizowekwa ili kuepusha ajali.

“Shirika linatoa pole kwa ndugu wa marehemu na Mwenyezi Mungu awape nafuu majeruhi ili waweze kuendelea na shughuli za kujenga Taifa, taarifa zaidi zitaendelea kutolewa,” amesema.

spoti pesa below post

Global Publishers and General Enterprises Limited is a registered private company dealing in publishing of weekly Swahili newspapers in Tanzania, namely; Uwazi, Ijumaa, Championi, Amani, Risasi & Ijumaa Wikienda.