Tanzania
This article was added by the user . TheWorldNews is not responsible for the content of the platform.

Yanga Yashtukia Mtego Wapinzani Wao Al Merrikh Ligi ya Mabingwa Afrika

JANA Jumatano Al Merrikh wametua Dar kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Yanga, Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe, amechimba mkwara mzito kuwa wameshtukia mtego wa wapinzani wao hao.

Jumamosi ya wiki hii kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar, timu hizo zitavaana ukiwa ni mchezo wa mkondo wa pili ambapo mshindi wa jumla anatarajiwa kukata tiketi ya kutinga hatua ya makundi ya mashindano hayo.

Ikumbukwe kwamba, mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa nchini Rwanda, uliisha kwa Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 0-2.

Akizungumza na Spoti Xtra, Kamwe alisema: “Tumesikia maneno mengi kutoka kwa kocha wa Merrikh akisema Yanga inaogopwa Afrika na kuwa watakuja kucheza kwa kushambulia ili kupindua matokeo.

“Lakini niwaweke wazi kuwa sisi kama Yanga tumeshashtukia mbinu hiyo na hatutaingia mtegoni kwa matumizi ya propaganda zao, tunajua kuwa kazi haijaisha, hivyo hatutaingia kwa kujisahau kutokana na sifa tunazopata bali tutapambana kuandika historia.”

Hivi karibuni, Kocha wa Al Merrikh, Osama Nabieh, aliisifia Yanga kwa kiasi kikubwa akisema timu hiyo ni miongoni mwa timu bora kwa sasa kulingana na ubora ambao wanazidi kuuonesha.

spoti pesa below post

Global Publishers and General Enterprises Limited is a registered private company dealing in publishing of weekly Swahili newspapers in Tanzania, namely; Uwazi, Ijumaa, Championi, Amani, Risasi & Ijumaa Wikienda.