Tanzania
This article was added by the user . TheWorldNews is not responsible for the content of the platform.

Moto Iraq: Maharusi Wote Wawili Wapoteza Maisha, Afisa wa afya Afunguka

 Naibu Mkuu wa Kurugenzi ya Afya ya Ninawi, Ahmed Dubardani.

Wanandoa hao wapya wote walipoteza maisha katika moto uliowaka katika karamu ya harusi nchini Iraq, kulingana na Ahmed Dubardani, naibu mkuu wa kurugenzi ya afya ya Ninawi.

Takriban watu 100 wamefariki na wengine 150 kujeruhiwa baada ya moto kuzuka kwenye harusi kaskazini mwa Iraq, vyombo vya habari vya serikali vimeripoti.

Akizungumza na wanahabari hapo awali katika mkutano na wanahabari, aliongeza kuwa takriban watu hamsini wako katika hali mbaya, na angalau nusu yao wameungua.

“Wengi wa waliojeruhiwa waliungua kabisa. Na wengine asilimia 50 hadi 60 ya miili yao iliungua. Hii si nzuri hata kidogo,” alisema.

Aliongeza kuwa wengi wa waliojeruhiwa walikuwa vijana wa kiume na wa kike – hakuna aliyeruhusiwa kuondoka hospitali kufikia sasa.

spoti pesa below post

Global Publishers and General Enterprises Limited is a registered private company dealing in publishing of weekly Swahili newspapers in Tanzania, namely; Uwazi, Ijumaa, Championi, Amani, Risasi & Ijumaa Wikienda.