Msanii wa filamu @wemasepetu amefunguka kueleza jinsi siku yake muhimu yakuzaliwa ilivyogeuka mwika katika yake ambayo imemfanya aape tutosherekea tena siku yake ya kuzaliwa.

Mwigizaji huyo ametoa taarifa hii “Nia na Madhumuni yangu ilikuwa ni kutaka kusherehekea siku yangu ya kuzaliwa n kuenjoy na wapenzi wangu ila haikuwa vile nilivyotarajia… Inshort shughuli yangu iliharibika sana… Lengo langu halikutimia… Nimejitahidi kufanya kitu kizuri ambacho kingenifurahisha sana siku ya Birthday yangu ila haijakuwa… … Najiskia vbaya sana… This was the worst Birthday Party of my Life nd nahisi sitokuja fanya Party tena kwenye maisha yangu… Naumia moyoni mwangu ila kila kitu kinatokea kwa sababu… Ndo maana acha tu niseme
“Alhamdulillah”. Had to take that off my chest… Ningekaa kimya ningekufa…”

Hatua hiyo imekuja baada ya hotuba ya Mama yake mazazi kuonekana kumkataa mpenzi wake Whozu mbele ya umati wa mastaa ambao walijitokeza.

Mama Wema alidai hapendezwi na mwanaume wake huyo ambaye ni msanii wa muziki jinsi anavyokaa nyumbani kwa mtoto wake bila utaratibu wowote.

Una mtazamo gani juu ya sakata hilo?

Photo of Yasini Ngitu