Tanzania
This article was added by the user . TheWorldNews is not responsible for the content of the platform.

Rais wa Rwanda Amteua Jenerali Mshukiwa kuwa Waziri

Rais wa Rwanda Paul Kagame amemteua afisa mkuu wa kijeshi kuwa waziri wa nchi kwa ushirikiano wa kikanda licha ya kwamba anashutumiwa kufanya kazi kwa karibu na kundi la waasi la Kongo.

Jenerali James Kabarebe, ambaye kwa miongo kadhaa amekuwa mshirika wa karibu wKagame, alistaafu kutoka jeshi mwezi uliopita.

Wataalamu wa Umoja wa Mataifa walichapisha ripoti mwezi Juni wakimtuhumu Jenerali Kabarebe kwa kuwa na jukumu kubwa katika kuratibu operesheni za kundi la waasi la M23 mashariki mwa DR Congo. Rwanda imekanusha kuwa jeshi lake limeunga mkono kundi la M23.

Tangu kundi hilo lianzishe tena uasi karibu miaka miwili iliyopita, mamia ya maelfu ya raia wamelazimika kuyahama makazi yao.

DR Congo inaishutumu Rwanda kwa kuunga mkono M23 – madai ambayo yamekanushwa mjini Kigali.

spoti pesa below post

Global Publishers and General Enterprises Limited is a registered private company dealing in publishing of weekly Swahili newspapers in Tanzania, namely; Uwazi, Ijumaa, Championi, Amani, Risasi & Ijumaa Wikienda.