Tanzania
This article was added by the user . TheWorldNews is not responsible for the content of the platform.

Uganda Yawasimamisha Kazi Wafanyikazi 11 juu ya Vibali Bandia vya Sokwe

Mamlaka ya wanyamapori nchini Uganda imewasimamisha kazi wafanyikazi wake 11 kwa tuhuma za uuzaji wa vibali feki vya sokwe.

Wakala wa serikali, ambao huuza vibali vinavyowaruhusu watalii kuwaona sokwe kwa karibu, ilisema imepata hitilafu katika shughuli zake za mtandaoni.

Kampuni za Safari zinasema kuwa kibali kwa sasa kinagharimu takriban $700 (£575) kwa kila mtu kwa safari – na idadi ndogo hutolewa kila mwaka.

Kulingana na gazeti la kibinafsi la Daily Monitor la Uganda, wakaguzi walibaini kuwa idadi ya wageni katika mbuga za Mgahinga na Bwindi hailingani na mapato yaliyokusanywa.

Bashir Hang, msemaji kutoka Mamlaka ya Wanyamapori Uganda (UWA), alisema uwezekano uchunguzi unafanywa kubaini iwapo wafanyakazi na waongozaji wa watalii walifanya walishirikiana kutekeleza udanganyifu.

Shirika hilo liliongeza kuwa bado halijabaini ni pesa kiasi gani limepoteza katika wizi huo unaodaiwa.

Baadhi ya vigogo wa UWA wanatarajiwa kuhojiwa kuhusu kashfa hiyo, gazeti la serikali la New Vision lilisema.

Sokwe huzalisha mapato makubwa ya utalii kwa Uganda, na baadhi ya pesa huenda kwenye juhudi za uhifadhi wa wanyamapori.

spoti pesa below post

Global Publishers and General Enterprises Limited is a registered private company dealing in publishing of weekly Swahili newspapers in Tanzania, namely; Uwazi, Ijumaa, Championi, Amani, Risasi & Ijumaa Wikienda.