Mwalimu James Kidiga wa shule ya sekondari Kiara Musoma Manispaa Mkoani Mara ameingia kwenye orodha ya walimu 50 bora duniani (the Top 50 Finalist for the Global @teacherprize 2023 organized by Varkey Foundation & UNESCO).

Hatua hiyo ameifikia baada ya kupita katika mchujo wa waalimu 7000 duniani katika nchini 130 ambazo zilituma wawakilishi wake na kuwa Mwalimu pekee kutoka Tanzania katika kinyang’anyiro hicho.

Kidiga ambaye ni mwalimu kwa miaka 9, pia ni mratibu wa chama cha walimu wa kiingereza (Tanzania English Language Teachers’ Association – TELTA) Mkoa wa Mara.

Mwaka 2022, alikuwa ni mmoja kati ya walimu wanne walioalikwa bungeni Dodoma na Waziri wa Elimu, Mh. Adolf Mkenda baada ya kushinda program ya Fulbright TEA.

Kupitia taarifa yake amesema “Napenda kuhamasisha walimu wenzangu kuchangamkia fursa mbalimbali licha kuwa na changamoto kadha wa kadha makazini kwetu ila tusisahau kuishi kwa kujaribu fursa kama hizi huku tukiendelea kuzalisha wahitimu bora mashuleni.,”

Written by @yasiningitu

Photo of Yasini Ngitu