Tanzania
This article was added by the user . TheWorldNews is not responsible for the content of the platform.

Magari taasisi za umma, binafsi zatakiwa kufanyiwa ukaguzi NIT

Naibu Waziri Kihenzile ametoa wito kwa taasisi za umma na binafsi kufanya ukaguzi wa magari yao mara kwa mara ili kupunguza matukio ya ajali za barabarani.

Akizungumza jijini Dar es Salaam mara baada ya kutembelea miradi mbalimbali ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (Tanesco, Kihenzile amesema ni muhimu kwa taasisi hizo kufanya ukaguzi wa magari na kuweza kuwaapisha ili kupunguza matukio ya ajali za barabarani.

“Kwa kuzingatia ajali za barabarani zinazidi kutokea kila kukicha niwaombe waje kukagua magari teyu ili yanapotembea barabarani yaweze kuwa na ubora kwa lengo la kunusuru maisha ya raia,” amesema

Kwa upande wake, Mkuu wa chuo hicho, Profesa Zakaria Mganilwa amesema kituo cha ukaguzi wa magari kilijengwa kwa ajili ya wanafunzi wao, maofisa wa polisi wanaohusika na ukaguzi na maofisa wa bima.

Amesema wanachokifanya maofisa wa bima ni kuthamanisha gari baada ya kupata ajali na kisha kuwalipa wateja wao.

“Tumekuwa tukihamasisha umma walete magari yao Ili kujua ubora wake kwani tunakagua zaidi ya mifumo 15 hasa inayoendana na usalama wa gari,”amefafanua.

Profesa Mganilwa amesema watu ambao wanauziana magari pia Wana wajibu wa kupeleka magari hayo kufanyiwa ukaguzi kabla ya kununua ili likaguliwe na watapewa taarifa ya gari husika.

“Baada ya ukaguzi tutatoa ripoti ambayo huenda mnunuzi badala ya kununua kwa Shilingi milioni nane unaweza kuambiwa gari inahitaji matengenezo ya milioni 12 hivyo ukajikuta unanunua gari kwa milioni 20,” amesisitiza.

Amesisitiza kuwa wanahamasisha watanzania watumie kituo hicho kwani ukaguzi wa gari dogo huanzia Sh 60,000 huku gharama ya magari makubwa hutegemea na mahitaji na kwamba kituo hicho kitawasaidia kuwa na uhakika wa kupunguza ajali za barabarani.