Tanzania
This article was added by the user . TheWorldNews is not responsible for the content of the platform.

Rais wa Zambia Ashukuru Rais Samia Kuipa nchi hiyo hekta 20 za ardhi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akikaribishwa Ikulu Jijini Lusaka na mwenyeji wake Rais wa Zambia Hakainde tarehe 25 Oktoba, 2025.

Rais Hakainde Hichilema wa Zambia amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuipa nchi hiyo hekta 20 za ardhi kwa ajili ya kuhudumia mizigo ya nchi hiyo.

Rais Hichilema amesema hayo wakati wa mkutano na waandishi wa habari alioufanya na Rais Samia kwenye Ikulu ya Zambia iliyopo jijini Lusaka.

Rais Hichilema alisema Wazambia wamechukua hatua hiyo kama zawadi ya kuonyesha ushirikiano mwema baina ya nchi hizi mbili.

Katika hotuba yake kama mgeni rasmi wa maadhimisho ya miaka 59 ya Uhuru wa Zambia yaliyofanyika jana jijini Lusaka, Rais Samia alisema eneo ambalo Zambia itapewa liko Kwala, mkoani Pwani.

Rais Samia akikaribishwa Ikulu Jijini Lusaka na mwenyeji wake Rais wa Zambia Hakainde tarehe 25 Oktoba, 2025.
Rais Samia akiwa kwenye picha ya pamoja na mwenyeji wake Rais wa Zambia Mhe. Hakainde Hichilema mara baada ya kuwasili Ikulu ya Lusaka nchini Zambia tarehe 25 Oktoba, 2025
Rais Samia akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu ziara yake ya Kitaifa Lusaka nchini Zambia mara baada ya mazungumzo yake na Rais wa nchi hiyo Mhe. Hakainde Hichilema tarehe 25 Oktoba, 2025
Rais wa Zambia  Hakainde Hichilema akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu Ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan nchini humo tarehe 25 Oktoba, 2025
spoti pesa below post

Global Publishers and General Enterprises Limited is a registered private company dealing in publishing of weekly Swahili newspapers in Tanzania, namely; Uwazi, Ijumaa, Championi, Amani, Risasi & Ijumaa Wikienda.