Tanzania
This article was added by the user . TheWorldNews is not responsible for the content of the platform.

Tanesco Ubungo yatakiwa kushughulia tatizo la kukosekana kwa umeme

Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kituo cha Ubungo kimepewa saa sita kuhakikisha wanashughulikia tatizo la kukosekana kwa umeme.

Hayo yamebainishwa leo na Naibu Waziri wa Nishati, Judithi Kapinga wakati akitoa maelekezo kwa watendaji wa shirika hilo mara baada ya kutembelea na kukagua mitambo ya umeme iliyopo Ubungo jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri Kapinga amesema anafahamu kuwa kituo cha Ubungo 1 kilizimika umeme tangu jana usiku huku jitihada za kurejesdha uzalishaji zikiendelea hivyo wananchi wasiwe na wasiwasi.

Amesema kwenye kituo hicho cha Ubungo 1 kuna mashine tat una mbili ndizo zinafanya kazi huku moja haifanyi kazi na ipo kwenye matewngenezo.

“Kituo cha Ubungo 2 kina mashine 12 na sita kati ya hizo hazifanyi kazi ziko kwenye matengenezo lakini hizo sita zinazofanya kazi ndio zimezimika,” amesema Naibu Waziri Kapinga

Aidha amesema kuwa mashine zilizoharibika zina uwezo wa kuzalisha umeme wa Megawati 43 kila moja, ni umeme mwingi sana hivyo wanaimani kuwa kama matengenezo yatakamilika kwa wakati hali ya upatikanaji wa umeme itaimarika.

Wafanyakazi Tanesco watakiwa kuwa na mipango ya kufanya marekebisho mitambo ya umeme

Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amewataka wafanyakazi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kuhakikisha wanakuwa na mpango Madhubuti wa kufanya marekebisho ya mitambo ya umeme mara kwa mara.

Kapinga ameyasema hayo leo Ijumaa jijini Dar es Salaam wakati akitoa maelekezo kwa watendaji wa shirika hilo mara baada ya kutembelea na kukagua mitambo ya umeme iliyopo Ubungo jijini Dar es Salaam.

Amesema ni muhimu matengenezo ambayo yanapaswa kufanyika kwa muda mfupi yakamilike kwa wakati ili watanzania waweze kupata umeme wa uhakika.

“Kama wizara tunaendelea kuyafanyia kazi maelekezo ambayo yametolewa na Rais wa Tanzania Samia Suluhu ya kuhakikisha keri ya kukatika kwa umeme inakoma ndani ya miezi sita ikiwemo kutengeneza mashine zilizoharibika,” amesema

Written by Janeth Jovin