Tanzania
This article was added by the user . TheWorldNews is not responsible for the content of the platform.

Marekani imemkatalia waziri wa mambo ya nje wa Iran, kutembelea Washington

Hossein Amir-Abdollajian

Marekani, Jumatatu imesema ilikataa maombi ya waziri wa mambo ya nje wa Iran, ya kutembelea Washington, wiki iliyopita sababu ikiwa ni wasiwasi wa rekodi ya Tehran ikijumuisha kushikiliwa kwa raia wa Marekani siku za nyuma.

Waziri wa mambo ya nje Hossein Amir-Abdollajian, aliripotiwa kutaka kusafiri kutembelea ofisi ya ubalozi baada ya baraza kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani, Matthew Miller, aliwaambia wanahabari kwamba waliwasilisha maombi yake lakini yalikataliwa na wizara.

Amesema kwamba hawana jukumu la kuruhusu maafisa wa Iran na mataifa mengine wa serekali kusafiri kwenda New York kwa shuguli za Umoja wa Mataifa, lakini linapokuja suala la kuja Washington, jukumu hilo ni la kwao.

Iran wiki iliyopita iliwaachilia raia watano wa Marekani kutoka gerezani kwa kubadilishana na kuachiliwa dola bilioni 6 za Iran kutoka Korea Kusini katika akauti yake ya Qatar.

spoti pesa below post

Global Publishers and General Enterprises Limited is a registered private company dealing in publishing of weekly Swahili newspapers in Tanzania, namely; Uwazi, Ijumaa, Championi, Amani, Risasi & Ijumaa Wikienda.