Tanzania
This article was added by the user . TheWorldNews is not responsible for the content of the platform.

Kocha wa Yanga Atamba Kumaliza Kazi dhidi ya Al Merrikh ya Sudan

Global Publishers and General Enterprises Limited is a registered private company dealing in publishing of weekly Swahili newspapers in Tanzania, namely; Uwazi, Ijumaa, Championi, Amani, Risasi & Ijumaa Wikienda.

Miguel Gamondi

KOCHA Mkuu wa Yanga, Muargentina, Miguel Gamondi, ameibuka na kutamka kwamba, amekamilisha maandalizi ya kikosi chake kwa asilimia mia moja, hivyo yupo tayari kupata ushindi na kuandika rekodi ya kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika watakapocheza dhidi ya Al Merrikh ya Sudan.

Timu hizo zinatarajiwa kuvaana keshokutwa Jumamosi ukiwa ni mchezo wa marudiano wa kuwania kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika utakaochezwa Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

Katika mchezo wa kwanza, Yanga ilipata ushindi wa mabao 0-2 ugenini, kwenye Uwanja wa Pele, Kigali, Rwanda.

Akizungumza na Spoti Xtra, Gamondi alisema amekifanyia marekebisho ya kutosha kikosi chake, kwa kuboresha baadhi ya sehemu zenye upungufu ili kuhakikisha wanapata ushindi utakaowapeleka hatua ya makundi.

Gamondi alisema wapinzani wao ni wazuri katika fitinesi, wakicheza soka la kutumia nguvu nyingi, hivyo katika mchezo huo ataingia na mbinu nyingine zitakazomuwezesha kupata ushindi.

Aliongeza kuwa, ili kuhakikisha wachezaji wake wanaendana na aina ya soka hilo la nguvu, amewapa mazoezi magumu ya gym, kimbinu na ufundi kwa lengo la kupata matokeo mazuri sambamba na kuwapa burudani mashabiki.

“Nimekamilisha maandalizi yangu, kuelekea mchezo ujao dhidi ya Al Merrikh, vijana wangu nimewapa mbinu zitakazotuwezesha kupata ushindi katika mchezo huo.

“Ninataka kuona timu yangu ikicheza soka safi la pasi kwa spidi, pia tukipata ushindi mkubwa kwa lengo la kuwapa furaha mashabiki wetu,” alisema Gamondi.

STORI NA WILBERT MOLANDI

spoti pesa below post