Beki wa Klabu ya Simba, Che Fondoh Malone amepata ajali ya gari usiku wa kuamkia leo akitokea Airport ya Kimataifa ya Mwalimu Julius Nyerere kutoka kuwapokea ndugu zake.

Ajali hiyo imemkuta maeneo ya Mikocheni alipokuwa akirejea nyumbani baada ya kuwapokea kaka zake Airport.

Kwa mujibu wa Meneja Habari wa Simba, Ahmed Ally gari lilikuwa likimkwepa Bodaboda na kujikuta wakiingia Mtaroni.

Inadaiwa gari alilopanda lilikuwa na abiria wanne akiwemo yeye na hakuna aliyepata majeraha makubwa.

Che Malone ambaye alikuwa dereva kwenye gari hilo dogo hajaumia na anatarajiwa kuungana na wachezaji wenzake hapo kesho kwenye mazoezi.

Photo of Hamza Fumo