Tanzania
This article was added by the user . TheWorldNews is not responsible for the content of the platform.

Bingwa wa Shigongo Cup, Kupatikana leo Septemba 9 Uwanja wa Nyanzenda, Buchosa

Global Publishers and General Enterprises Limited is a registered private company dealing in publishing of weekly Swahili newspapers in Tanzania, namely; Uwazi, Ijumaa, Championi, Amani, Risasi & Ijumaa Wikienda.

Mbunge wa Buchosa, Erick Shigongo.

BINGWA wa mashindano ya Shigongo Cup, anatarajiwa kupatikana  leo Septemba 9, 2023 ,katika mchezo wa fainali itakayopigwa kwenye Uwanja wa Nyanzenda uliopo Jimbo la Buchosa, Wilayani Sengerema mkoani Mwanza.
Fainali huyo inatarajiwa kuzikutanisha timu za Kata ya Nyanzenda dhidi ya timu ya Kata ya Bupandwa.

Bingwa wa mashindano hayo anatarajiwa kuzoa kiasi cha shilingi milioni moja na kombe, mshindi wa pili atapata shilingi laki tano na mshindi wa tatu shilingi laki tatu.


Pia kutakuwa na zawadi zingine kama mfungaji bora, mchezaji bora na kipa bora kila mmoja atapata tuzo na shilingi laki moja, huku zawadi mbalimbali zitatolewa kwa vikundi vya mashabiki.
Mashindano hayo maalum yanaendelea katika Jimbo la Buchosa wilayani Sengerema mkoani Mwanza, ambapo yalianza kwa kushirikisha timu 22 na kuratibiwa na Ofisi ya Mbunge wa Buchosa, Erick Shigongo.
Timu hizo 22 zilipangwa katika makundi manne, Kundi A lilizikutanisha timu kutoka Kata ya Nyanzenda, Kasisa, Nyakasungwa, Kalebezo, Bukokwa na Nyehunge.
Kundi B liliundwa na kata ya Buhama, Bugoro, Nyakasasa na Lugata. Kundi C lilizikutanisha kata ya Luharanyonga, Bulyaheke A, Bulyaheke B, Irenza, Kazunzu na Nyakarilo na kwa upande wa Kundi D zilipangwa timu za kata ya Kafunzo, Irigamba, Bangwe, Maisome, Katwe na Bupandwa.
Mratibu wa kamati ya mashindano hayo, Marco Zagalo, amesema mashindano hayo yamekuwa
na kasi na ushindani mkubwa kutokana na vijana kuonesha vipaji vya hali ya juu na mwamko kutoka kwa mashabiki wao ambao wanajitokeza kwa wingi kushangilia timu zao.
“Tumekuwa na mashindano bora kwani tunaona ushindani uliopo kwa timu zote tukiangalia vipaji vilivyopo kila timu na mwamko mkubwa wa mashabiki kujitokeze viwanjani kushangilia timu zao hii inaonyesha mashindano haya yataleta faida kubwa sana kwa Jimbo letu la Buchosa chini ya mbunge wetu, Eric Shigongo kwa namna alivyojitoa kuhakikisha mashindano haya yanafanyika kila mwaka,” alisema Zagalo.

spoti pesa below post