Tanzania
This article was added by the user . TheWorldNews is not responsible for the content of the platform.

Davido amekosa imani na watu wake wa karibu, shuhudia alichokifanya

Moja ya video inayosambaa mitandaoni ni hii ya Staa wa Muziki kutoka nchini Nigeria Davido ambayo inaonyesha kama amekosa imani na watu wake wa karibu.

Wengi wanaeleza kuwa Davido siku hizi hawaamini kabisa watu wake wa karibu na hii imeanzia baada ya video ikimuonyesha akikataa maji ya kunywa aliyopewa na mlinzi wake siku ya maandamano ya msanii aliyefariki dunia Mohabd huko Lagos.

mbali na hilo inaelezwa kuwa ameongeza ulinzi zaidi kwa sasa ikielezwa kuwa kuna wasiwasi ameupata baada ya kusikia story za kifo cha Mohbad ambapo inaelezwa kama watu wake wa karibu ndio wamehusika kwa asilimia kubwa kwenye kifo chake.

Video hii inamuonyesha Davido akikataa chakula alichopakuliwa na watu wake wa karibu ambapo amempatia mtu mwingine na yeye kupakua chakula chake mwenyewe.

Watu wengi wanaeleza kuwa sio kawaida ya Davido kwani mara nyingi sio tu chakula hata vinywaji hushikiwa na kuwekewa na watu wake wa karibu, kama ana kitu anafanya basi kinywaji chake humpatia mlinzi wake au mtu yoyote wa crew yake.

Sasa hivi ameonekana kuwa na wasiwasi zaidi na kukosa imani kabisa na watu wake wa karibu kama inavyoonyesha kwenye video hii.

Davido kumpatia chakula chale rafiki yake ni sajihi??? Na Je Wewe mtu wake wa karibu unayemuamini sana ni nani???

Davido amekosa imani na watu wake wa karibu, shuhudia alichokifanya https://t.co/IeSpyCDS4R pic.twitter.com/5iOdTwNzNk

— bongo5.com (@bongofive) September 26, 2023