Hoteli ya Cristiano Ronaldo nchini Morocco imekua hifadhi ya manusura wa tetemeko la ardhi iliyoikumba nchi hiyo.

Pestana CR7 Marrakech Hoteli inayomilikiwa na Ronaldo imefungua milango yake kwa wahanga wa tetemeko hilo nchini Morroco.

Siku ya Ijumaa tetemeko kubwa la ardhi la kipimo cha 6.8 lilipiga eneo la milima ya High Atlas nchini Morocco, karibu maili 45 kutoka mji wa Marrakech.

Hadi kufikia jana jioni siku ya Jumamosi zaidi ya watu 1,305 wameripotiwa kufa kutokana na tetemeko la ardhi na wengine wengi kujeruhiwa au kutoweka.

Makampuni na wafanyabiashara mbalimbali kutoka nchi hiyo wameendelea kutoa misaada ikiwemo hoteli ya Mshambuliaji huyo wa Ureno na Al Nassr ikitoa makazi.

Photo of Hamza Fumo

Related Articles