Tanzania
This article was added by the user . TheWorldNews is not responsible for the content of the platform.

Jeshi La Polisi Latoa Tamko, Sakata La Kupotea Kwa Mtoto Warda – Video

Jeshi la Polisi Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani lilipokea taarifa ya kutoweka kwa mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Nyumbu, Warda Machamula (16) tangu Aprili 19, 2023.

Jeshi la polisi Mkoa wa Pwani lilianza kaye ya kutafuta chanzo cha kutoweka kwa motto huyo na ikagundulika kuwa mlezi aliyekuwa anaishi naye alimpiga ndiyo maana motto aliamua kutoroka (Jina limehifadhiwa).

Aidha Jeshi la polisi limeendelea kueleza kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa na baadaye kuachiwa kwa dhamana kwa mujibu wa sheria za makosa ya jinai.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linaendelea na uchunguzi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ili mototo apatikane.

Aidha Jeshi la Polisi linatoa wito kwa vyombo vya habari kuendelea kuhabarisha jamii kwa yeyote atakayempata mtoto kutoa taarifa mara moja katika kituo cha polisi.

Lakini pia Jeshi hilo limetoa wito kwa wazazi na walezi kufuatilia mienendo ya watoto wao kwa ukaribu Zaidi.

Familia inaendelea kuomba kwa yeyote atakayemuona au mwenye taarifa za mahali alipo, awasiliane nao kwa namba za simu ambazo ni:

0656520998 au 0687003356.

spoti pesa below post

Global Publishers and General Enterprises Limited is a registered private company dealing in publishing of weekly Swahili newspapers in Tanzania, namely; Uwazi, Ijumaa, Championi, Amani, Risasi & Ijumaa Wikienda.