Tanzania
This article was added by the user . TheWorldNews is not responsible for the content of the platform.

Kimeumana: Chama Cha Walimu Wafungiana Mageti – Msajili Anusuru Mkutano Wafanyika -Video

Vuta nikuvute imeibuka mapema Leo Septemba 25, asubuhi jijini Dodoma baada ya wanachama CWT kuzuiwa kuingia ndani ya geti huku wakilalamikia kupotezewa muda kwani wametoka sehemu mbalimbali ndani ya nchi.

Sakata hilo lilianza wakati wajumbe wa Baraza Kuu walipoanza kuingia eneo la kikao katika ofisi za CWT Mtaa wana Jamhuri na kukuta Polisi wakitoa katazo hilo kuwa hakuna kuingia ndani.

Mkuu wa Polisi wa Kituo cha Polisi Dodoma, Joram Samson aliongoza kikosi cha polisi aliongoza polisi wenzake katika katazo hilo.

Hata hivyo baadhi ya wajumbe hao walionyesha kukasirishwa na katazo hilo kwani hawakujua wapi limetoka kwani polisi hawakusema nani kawaambia wafunge geti hilo.

spoti pesa below post

Global Publishers and General Enterprises Limited is a registered private company dealing in publishing of weekly Swahili newspapers in Tanzania, namely; Uwazi, Ijumaa, Championi, Amani, Risasi & Ijumaa Wikienda.