Tanzania
This article was added by the user . TheWorldNews is not responsible for the content of the platform.

Kocha Merrikh: Yanga Inaogopwa Afrika Atoa Tamko kufuzu Hatua ya Makundi

Osamah Nabieh.

KOCHA wa Al Merrikh, Osamah Nabieh amekiri kwa kusema kuwa Yanga ni moja kati ya timu ambayo inahofiwa kwa sasa barani Afrika kulingana na kile ambacho inakionyesha ndani ya uwanja haswa kutokana na kupata matokeo mazuri na kucheza mpira mzuri.

Kocha huyo anayokumbukumbu ya kupokea kichapo cha mabao 2-0 wakiwa nyumbani katika mchezo wa kwanza wa kuwania kufuzu kucheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Al Merrikh wanatarajiwa kurudiana na Yanga katika mchezo wa mzunguko wa pili wakiwa ugenini katika Uwanja wa Azam Comlex mchezo huo unatarajiwa kufanyika Septemba 30.

Akizungumza kuelekea katika mchezo wa marudiano dhidi ya Yanga kocha huyo alisema kuwa: “Ukisema kuwa tunahofia kukutana na Yanga hapana, hilo halina ukweli kwa kuwa tayari tulishacheza nao na tulipoteza mchezo wa kwanza, ukweli ni huu kuwa Yanga kwa sasa ni tishio Afrika kulingana na walivyo.

“Ni timu ambayo inacheza vyema na inapata matokeo hivyo ni lazima tuwaheshimu kulingana na ubora wao huo, tunakwenda kurudiana na timu ambayo ni ngumu lakini wakiwa na faida kubwa ya wao kucheza kwao.

“Ambacho kipo kwa upande wetu ni kuendelea kujipanga kwa ajili ya kuhakikisha kuwa tunafanya vyema, kuwa na mipango mizuri ya kupata matokeo tukiwa ugenini, nia na malengo yetu ni kwenda hatua inayofuata na tuna matumaini hayo na wala hatujakata tama,” alisema kocha huyo.

Na Marco Mzumbe

spoti pesa below post

Global Publishers and General Enterprises Limited is a registered private company dealing in publishing of weekly Swahili newspapers in Tanzania, namely; Uwazi, Ijumaa, Championi, Amani, Risasi & Ijumaa Wikienda.