Msanii mkongwe wa muziki wa BongoFleva @jidejaydee katika ahadi yake ya #MamboMatano ya mwezi huu, ametangaza nafasi ya kuwasomesha wanafunzi watano wa chuo mpaka Masters.

“Jambo la tatu kati ya #MamboMatano toka kwangu ni nafasi za masomo kwa wanafunzi watano wa chuo. Haijalishi jinsia, ila kwa kipaumbele watachukuliwa wasichana 3 na wavulana 2.,” Taarifa hiyo na LadyJayDee ilieleza.

Aliongeza, “Ni kwa wawe watu ambao hawana uwezo kabisa wakulipiwa na mzazi
na watasomeshwa mpaka Masters hata kama waliishia njiani watasaidiwa kuendelea. Lakini uwezo wa akili pia ni kigezo lakini kikubwa wawe hawana uwezo,”

Muimbaji huyo ambaye hajawahi kushuka kwenye muziki wake, yeyote ambayo anaona anataka nafasi hizo atume taarifa [email protected].

Written and edited by @yasiningitu

Photo of Yasini Ngitu

Related Articles