Tanzania
This article was added by the user . TheWorldNews is not responsible for the content of the platform.

Mamia Wafariki Kwa Denge na Kipindupindu Sudan, Hospitali Zafungwa!

Mlipuko wa homa ya Denge, na Kipindupindu kutokana na ukosefu wa maji umeua mamia ya watu katika taifa lenye vita Sudan, ripoti za wataalamu wa afya zimeeleza Jumatatu, na kutoa onyo kwa mlipuko huo kusambaa zaidi kutatiza mfumo wa afya ulio mashakani.

Katika taarifa, chama cha madaktari wa Sudan kimeonya kwamba hali ya afya katika jimbo la kusini mashariki la Gedaref, kwenye mpaka na Ethiopia, imekuwa mbaya kwa kiwango kikubwa ambapo maelfu wameambukizwa homa ya Denge.

Japokuwa Gedaref haijapata athari za moja kwa moja za vita baina ya jeshi na vikosi vya akiba vya (RSF), imekubwa na mgogoro kutoka kwa watu waliokosa makazi na huduma za kibinadamu.

Zaidi ya miezi mitano katika vita, asilimia 80 ya hospitali za Sudan hazifanyikazi kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.

Hata kabla ya vita, sekta ya afya isiyo madhubuti ilikuwa na wakati mgumu kukabiliana na milipuko ya magonjwa ya kila mwaka inayo endana na msimu wa mvua kuanzia Juni ikijumuisha na Malaria na Denge.

spoti pesa below post

Global Publishers and General Enterprises Limited is a registered private company dealing in publishing of weekly Swahili newspapers in Tanzania, namely; Uwazi, Ijumaa, Championi, Amani, Risasi & Ijumaa Wikienda.