Tanzania
This article was added by the user . TheWorldNews is not responsible for the content of the platform.

Meya wa mji wa Derna nchini Libya amekamatwa pamoja na maafisa wengine

Ofisi ya mwanasheria mkuu yenye makao yake katika mji mkuu Tripoli, imesema imetoa amri ya kuwazuia maafisa wanane wa eneo hilo kuhusiana na kupasuka kwa mabwawa katika dhoruba ambayo ilisababisha mafuriko yaliyoyasukuma maeneo na kuingia baharini na kuua maelfu ya watu.

Meya wa mji wa Derna mashariki mwa Libya alikamatwa pamoja na maafisa wengine kwa tuhuma za usimamizi mbaya na uzembe juu ya kupasuka kwa mabwawa yaliyofurika katika mji huo wiki mbili zilizopita, ofisi ya mwanasheria mkuu wa Libya imesema Jumatatu.

Ofisi ya mwanasheria mkuu yenye makao yake katika mji mkuu Tripoli, imesema imetoa amri ya kuwazuia maafisa wanane wa eneo hilo kuhusiana na kupasuka kwa mabwawa katika dhoruba ambayo ilisababisha mafuriko yaliyoyasukuma maeneo na kuingia baharini na kuua maelfu ya watu.

Wale waliokamatwa ni pamoja na meya na afisa anayesimamia rasilimali za maji, ilisema taarifa bila kuwataja majina. Wakazi wenye hasira wameilaumu mamlaka kwa kupasuka kwa mabwawa hayo ambayo yalikuwa yamejengwa ili kuzuia mtiririko wa maji katika mto mjini humo.

spoti pesa below post

Global Publishers and General Enterprises Limited is a registered private company dealing in publishing of weekly Swahili newspapers in Tanzania, namely; Uwazi, Ijumaa, Championi, Amani, Risasi & Ijumaa Wikienda.