Moja ya tukio la kusikitisha na kukemewa vikali ni hili kutoka nchini Ireland ambapo tukio hili linaonyesha mmoja ya watoto ambaye ni mweusi walioshinda/kushiriki kwenye moja ya mashindano nnchini humo kunyimwa medali  huku wenzake mweupe wakipewa medali zao.

Watu wengi wamelaani tukio hili kwani linaonyesha fika namna ubaguzi unavyoendelea kuyatafuna mataifa ya Ulaya kwa kupitia watu baadhi, mara nyingi wanaobaguliwa ni watu weusi.

Tukio hili vinasikitisha sana ukimuagalia Mtoto mweusi akisubiri medali bila bila mafanikio huku akiangalia wenzake wakipewa medali zao, mwishoni anaonekana kuongea na mwenzake labda akimuuliza mbona mimi sijapewa Medali?

Unahisi nini kifanyike kukomesha tabia hizi za Ubaguzi wa rangi??

Photo of Ally Juma