Tanzania
This article was added by the user . TheWorldNews is not responsible for the content of the platform.

Naibu Waziri Mkuu Doto Biteko – “Badilisha Santuri Ya Hii Wizara, Isiwe Wizara Ya Migogoro” – Video

Global Publishers and General Enterprises Limited is a registered private company dealing in publishing of weekly Swahili newspapers in Tanzania, namely; Uwazi, Ijumaa, Championi, Amani, Risasi & Ijumaa Wikienda.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Doto Biteko ameiagiza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kufanyia kwa ufanisi majukumu yake ya msingi ambayo ni kupanga, kupima na kumilikisha ardhi ili kuondoa migogoro ya ardhi inayotokea nchini na kuifanya Wizara husika kuishughulikia mara kwa mara.

Ameyasema hayo tarehe 9 Septemba, 2023 jijini Dodoma wakati wa hafla ya kuzindua kituo cha Taifa cha Ubunifu na Mafunzo ya taarifa za kijiografia kwa niaba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

“ Kazi za Wizara hii ni tatu, ambazo ni kupanga, kupima na kumilikisha ardhi, sasa tujipime na tujitathmini kama katika sekta yetu ya ardhi kazi hizi tunazifanya kwa ukamilifu wake, lipo wimbi la kuweka tension ya Wizara kutoka kwenye Sheria yake au Ilani ya uchaguzi na kugeuka kuwa Wizara ya utatuzi wa migogoro ya ardhi; kuanzia sasa tuwafanye watanzania wazungumze mipango miji, maendeleo ya makazi na matumizi bora ya ardhi.” Amesisitiza Dkt. Biteko

Ameitaka Wizara hiyo pia kushirikiana na Halmashauri zote nchini ili kazi zifanyike kwa ufanano na hivyo kwa pamoja waweze kuondoa urasimu na kuondoa migogoro ya ardhi na hivyo ana imani kuwa Wizara hiyo itamaliza changamoto zilizopo na kuweza kupanga miji ipasavyo na kuimarisha makazi ya watu ili kujenga Tanzania iliyo bora zaidi.

“Wizara hii ni moyo wa shughuli za uchumi hapa nchini, kwani watu wanaofanya shughuli za ujenzi, kilimo, wanaojenga miradi mbalimbali ikiwemo ya gesi asilia, wanategemea Sekta ya Ardhi, pamoja na kazi kubwa iliyofanyika ya kuimarisha sekta hii bado kuna kazi kubwa mbele ya kujiimarisha.”Amesema Dkt. Biteko

Kuhusu kituo hicho alichokizindua, Dkt.Biteko amesema kuwa, ni muendelezo wa hatua zinazochukuliwa na Rais, Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kuchochea matumizi ya teknolojia katika kuleta maendeleo endelevu na ubunifu hapa nchini.

Amesema kuwa kituo hicho ni muhimu kwani kitaboresha shughuli za upimaji ardhi, uandaaji wa ramani za msingi, ujenzi wa miundombinu, kupanga matumizi bora ardhi pamoja na masuala mengine yanayohusiana na Sekta ya Ardhi.

spoti pesa below post