Tanzania
This article was added by the user . TheWorldNews is not responsible for the content of the platform.

Nane Simba SC hawajapata nafasi ya kucheza

Klabu ya Simba SC msimu huu mpya 2023/24 mpaka sasa imecheza michezo Saba ya ushindani kuanzia Ngao ya jamii michezo miwili dhidi ya Singida Fountain gate pamoja na Yanga na Simba kushinda Ngao ya jamii kwa kutwaa Ngao ya jamii,wamecheza mchezo mmoja wa ligi wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya power Dynamos pamoja na michezo mitatu ya ligi kuu soka Tanzania Mtibwa Sugar,Dodoma Jiji pamoja na Coastal Union na hawajapoteza michezo hata mmoja.

Katika michezo hiyo Saba ya kimashindano rasmi Kuna wachezaji 8 wanyama mpaka sasa hawajapata nafasi ya kucheza mchezo wowote wachezaji wenyewe ni

1- Shaban Idd Chilunda
2- David Kameta ‘Duchu’
3- Abdallah Hamis
4- Jimmyson Mwanuke
5- Ahmed Feruz (GK)
6- Mohammed Musah
7- Nassor Kapama
8- HusseinAbel

Kundi kubwa la wachezaji Hawa mpaka sasa kushindwa kupata nafasi shida Nini ni kiwango au hawapo fiti? Nini Mtazamo wako?