Mshambuliaji wa Manchester city, Erling Haaland kupitia gazeti la L’Equipe amesema kuwa miaka 10 ijayo anatamani kuja kuwa Mchezaji wa tofauti na mwenye mataji mengi zaidi.

“Ni swali zuri. Ni wazi, ningependa kushinda mataji mengi na wachezaji wenzangu, lakini pia ningependa watu wanikumbuke kama mtu tofauti uwanjani, kwa jinsi ninavyocheza. Kwa hali yoyote, ndivyo ninavyojaribu kufanya kila wiki, kuonyesha kitu maalum, ikiwa unataka. Ndiyo, kutambuliwa kuwa mtu tofauti kungenifaa sana.”

Erling Haaland na Kylian Mbappé wanachukuliwa kama kizazi kitakachovunja Ufalme wa Messi na Ronaldo ambao umedumu kwa zaidi ya miaka 10.

Photo of Hamza Fumo

Related Articles