Cristiano Ronaldo na Lionel Messi licha ya kuwa hawapo tena kwenye Ligi kubwa duniani, lakini bado wamekuwa wakishindanishwa kila siku na mashabiki wa soka.

Akiwa kwenye mahojiano, Ronaldo amesema kuwa ushindani kati yao umekwisha ”Ushindani umekwisha. Sote tunafanya vizuri (Saudi na MLS).”

Kauli hii inahitimisha zama za mafahari hawa wawili waliyoupiga mwingi zaidi kwenye ulimwengu wa soka na kuzungumzwa kila kona ya Dunia.

Je, unajivunia kuwa miongoni mwa waliyoshuhudia kizazi cha Ronaldo na Messi.?

Photo of Hamza Fumo