Tanzania
This article was added by the user . TheWorldNews is not responsible for the content of the platform.

Sababu sita za soka la Bongo kukua na kupendwa

Wiki iliyopita mapema katika orodha ya viwango vya FIFA kumepanda kwa nafasi mbili kutoka 124 mpaka 122 kwa upande wa Soka la wanaume, Na ligi yetu kwa sasa inashika nafasi ya mpira 5 kwa ligi Bora barani Afrika kwa klabu zetu zikiendelea kufanya vizuri kimataifa kiufupi tunazidi kuendelea kwenye Football.

Nimefanya ufafiti wa muda mrefu kwa Nini soka letu linapiga sana hatua na Tanzania watu wanapenda sana mpira na hizi ndiyo sababu kuu kubwa.

1:AZAM TV wameusaidia sana mpira wa Tanzania kukua kwa kasi sababu watu Wana ufatilia baada ya Azam kuonesha maanake wamepadhisha hadhi na thamani kwa wadau na wadhamini kuja kwa wingi kuweka mzigo maanake watapata fusna ya kuonekana mfano kama NBC pamoja na Azam wenyewe maanake pesa wanazotoa zinasaidia kuendesha timu ivyo ushindani ukaanza kuongezeka.

2:Wadhamini walijitokeza kuweka pesa kla vilabu mfano wadhamini wa ligi kuu ya Tanzania au wadhamini wa klabu mfano Singida Wana udhamini kama 8 ndiyo maana wananguvu ya kusajili wachezaji Bora na kuwasaidia kujiendesha bila kuteteleka .

3: Uongozi Bora na Utawala Bora katika vilabu vingi kwa sasa viongozi wao wanajitahidi kuendesha Kisasa na kitaalam tofauti na miaka ya nyuma pia wanaendana na wakati pamoja na ushindani ukubwa uliopo maana Mpira kwa sasa ni biashara kubwa kwa sasa ,ndiyo unaona vilabu vingi kwa vinaajiri meneja wa Habari na Mawasiliano mfano Zaka zakazi wa Azam FC,Ahmed Ally ndani ya Simba SC pamoja na Ally Kamwe hao ni maafisa wa Habari katika vilabu vikubwa wanatoa habari,lakini pia wanaongeza thamani ya brand za vilabu vyao ivyo wanasaidia sana Soka kufatiliwa na mashabiki hadi nje ya nchi.

4:Wachambuzi Hawa ni watu wanaochambua kitaalam mchezo wa Soka na mwenendo wake kiujumla kama unavyofaham Mpira ni mchezo wa maoni lakini unazingatia utaalam sasa Hawa wamefanya soka kuvutia zaidi kwa sasa nchini Tanzania tofauti na mchezo wowote au mpira na kinachofanya kukua ni maoni Yao ambayo wanakuwa wanatofautiana katika Mitazamo Hali inayozua mijadala na kuwafanya watu kushindana kwa hoja ivyo watu kuwafanya watu kuwa busy na mijadala ya soka.

5: Mashabiki wa Dhahabu kabisa watu wanapenda sana Soka japo wengi wao hawajuhi mpira sana kitaalam wapo wamshabiki wanaamini mpira ni kushinda au kucheza vizuri tu hawajuhi kufanya vibaya ila timu ikifanya vizuri utajua Tanzania Kuna watu wanapenda soka watu wanajinyonga Kisa timu imefingwa watu wanakufa kwa furaha timu imeshinda hasa katika mechi za Dabi ,Yanga juzi wameweka rekodi ya kwenda mechi ya ugenini na magari mengi zaidi Hilo siyo jambo la kawaida usichulie poa ni mahaba makubwa unapoona CAF wamewapa Simba SC nafasi ya michuano ya African football league uzinduzi utakuwa Dar es salaam katika Dimba la uwanja wa Benjamin Mkapa ni sababu wanajua uwanja huo utakuwa full house hongera sana Kwa mashabiki wa Soka wa Tanzania Sema wajifunze sana mpira wasiendeshwe zaidi na hisia.

6:Online media/Instagram Mwanzo nilikwambia uwepo wa Azam TV umesaidia sana ila Hawa watu wa Online ndiyo wana chagiza sana Soka la bongo kufatiliwa linawapa fursa wadau,mashabiki,wachezaji,viongozi kutoa maoni na Mitazamo Yao lakini inamfanya watu kupata taarifa za timu zao lakini pia kuleta taarifa za kujenga na kusoma hili kuisaidia watu kujilekebisha pamoja na vitandao ya ya Instagram inasaidia sana kuleta mijadala na page zao kufatiliwa na watu tofauti ndiyo maana utaona klabu ya Yanga imeongoza mwezi Afrika nzima hiyo maanake inafatiliwa sana kwenye insta pia inafatiwa na Simba.

NB: Kila mtu anamchango muhimu Kila mtu acheze part yake vizuri