Tanzania
This article was added by the user . TheWorldNews is not responsible for the content of the platform.

Simba Kuwafungia Busta Wazambia, Mbrazili Asuka Mtego Mzito

KOCHA Mkuu wa Simba Mbrazili, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amesema wameutumia mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Coastal Union uliopigwa Alhamisi iliyopita kama sehemu ya kujiandaa na mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamos ya Zambia.

Robertinho ameweka wazi kuwa katika mchezo uliopita dhidi ya Coastal Union aliwatumia wachezaji wenye uzoefu, ili kuzidi kutengeneza maelewano baina yao kuelekea mechi dhidi ya Power Dynamos itakayopigwa Jumapili.

Simba Jumapili watashuka uwanjani na Dynamos katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika kusaka tiketi ya hatua ya makundi ya mashindano hayo, ikumbukwe mchezo wa kwanza ambao Simba walicheza ugenini nchini Zambia, Simba walipata matokeo ya sare mabao 2-2.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Robertinho alisema: “Tumeutumia mchezo dhidi ya Coastal Union kujiandaa na mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamos. Tulijua Coastal watatupa mechi ngumu ambayo itazidi kutuimarisha.

“Ukiangalia kikosi cha mchezo ule kwa kiasi kikubwa tumewatumia wachezaji wenye uzoefu ambao tunategemea kuwatumia dhidi ya Power Dynamos.”

Stori na Joel Thomas

spoti pesa below post

Global Publishers and General Enterprises Limited is a registered private company dealing in publishing of weekly Swahili newspapers in Tanzania, namely; Uwazi, Ijumaa, Championi, Amani, Risasi & Ijumaa Wikienda.