Tanzania
This article was added by the user . TheWorldNews is not responsible for the content of the platform.

Stamico Yatunza Mazingira Kwa Kupanda Miti

•  *Wanawake na Mama  Samia watunza miti 560*

• *Kuenzi uzinduzi Kampeni ya At 50*

• *Asisitiza matumizi ya chuma badala ya miti*

Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) leo septemba 25 , 2023vlimefanikiwa kupanda miti 340 ikiwa ni jitihada za kupambana na mabadiliko ya tabia nchi na uharibifu wa mazingira.

Shughuli ya upandaji miti  iliongozwa na  Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.Seleman Jafo ikiwa sehemu ya kutekeleza kampeni ya STAMICO na Mazingira ya Miaka 50 ya Shirika.

Sambamba na hapo Mhe.ameitaka STAMICO kutoa elimu kuhusu matumizi ya chuma badala ya magogo katika kuimarisha miamba wakati shughuli za uchimbaji mdogo wa madini zikifanyika.

Akielezea kuhusu agenda ya mkaa wa Rafiki Briquettes ,amesema kuwa Wizara ya Madinj kupitia  STAMICO imesaidia katika kutunza mazingira kipitia  mkaa Rafiki Briquettes.

Akizungumzia kuhusu uzalishaji wa mkaa mbadala Mhe.Jafo amelioongeza shirika hilo kwa kutekeleza kwa vitendo maagizo aliyoyatoa wakati wa Maadhimisho ya miaka 50 ya STAMICO.

Ameitaka STAMICO kuja na minutes nyingine ya kupeleka vitalu vya miti katika mashule ili ipandwe pamoja kuhudumiwa kama mnavyofanya leo kwa kufanya hivyo mtakuwa mnaendelea kupeleka mtandao wa miti na kuongeza idadi.