Asante Mungu tumefanikiwa kufuzu AFCON Ivory coast michuano itakayofanyika mwka 2024,ni mara ya tatu tunafanukiwa kufuzu mara kwanza ni 1980 tukaja kufuzu baada ya mwaka 2019 ni baada ya miaka 39 na sasa tumefuzu Tena 2023 ni jambo jema kama taifa.

Mtazamo wangu kwenye hiyo michuano ya AFCON nchini Ivory timu ya taifa ya Tanzania tutafanya vizuri sana kwa sababu kubwa mbili moja kwa sasa timu yetu Ina wachezaji wengi Vijana wenye ubora mkubwa mfano Dickson Job, Ibrahim bacca,Haji Mnoga,Bakari Nondo Mwamnyeto, Novatus Dismas hao tunazungimzia upande wa ulinzi wanacheza wanacheza vilabu ambavyo vinacheza michuano mikubwa ivyo uzoefu unaongezeka.

Kwa upande wa kati Mpaka mbele wapo wachezaji wengi Vijana ambao wapo kwenye kiwango Bora zaidi mfano Abdul Seleman ‘Sopu’,Kibu Dennis,Morice Abraham,Clemence Mzize maana kuwa na wachezaji Vijana maanake ni jambo zuri kwa taifa kuwa na wachezaji ambao watakaa kwa muda mrefu kwenye timu itasaidia sana kufanya vyema.

Credit by Issaya Dede

Photo of Hamza Fumo

Related Articles