Kupitia kweye kipindi chake cha RECAP & MANDO @el_mando_tz ameichambua ngoma ya mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva Komando Jide ya MAMBO MATANO ambayo imetoka siku kadhaa nyuma.

@el_mando_tz anasema kuwa baada ya kuisikiliza kwa makini ngoma hiyo amegundua kuwa kuna mambo mengi sana wasanii wa kizazi kipya bado wanapaswa kujifunza kwa makongwe huyo.

@el_mando_tz anasema kuwa kuna namna ya uandishi wa nyimbo wasanii wa kizazi hiki wanakwama kwani maeo mengi yamekuwa sio ya kisanii bali ya kuonyesha muziki wa sasa ni uhuni tu na sio sanaa ya kuelemisha jamii.

Baadhi yao wanaimba matusi sana kwenye nyimbo zao wakiamini wanendana na kizazi hiki kumbe sivyo, ukiisikiliza Mambo matao ya Jide unagundua muziki una nzuri kabisa ya kufikisha ujumbe.

Unakubaliana na @el_mando_tz kwa asilimia ngapi??

Photo of Ally Juma

Related Articles